Kuna miradi mikubwa ambayo lengo lake ni kuboresha hali za watu kwa miaka ijayo. Tulikuwa tunapiga siasa tukiikwepa aina hiyo ya miradi, umefika wakati hatuwezi kuendelea kuikwepa.
Mradi wa treni hatuwezi kuukwepa, lazima nchi ifunguke. Ifike wakati liwe ni jambo la kawaida kwa mtu kufanya kazi Dar akiwa anaishi Dodoma au Singida.
Ujerumani mtu anafanya kazi Ulm ambako ni karibu na mpaka wa Switzerland lakini anaishi Hamburg ambako ni kaskazini kabisa. Lazima Tanzania tuifungue, sio sehemu kubwa ya nchi ibakie pori tu, mahali ambapo hakuna uhai wa kimaendeleo.