Wakati report zikidai Falcao kadanganya umri, huko England mshambuliaji mahiri wa Newcastle United, Pappis Cisse ambaye amekataa kuvaa jezi ya club yake yenye nembo ya Wonga, kampuni ya kukopesha pesa, alipigwa picha akiwa casino inayoitwa Aspers mwaka jana mwezi November
Cisse alikataa kuvaa jezi zenye nembo ya hiyo kampuni kwa sababu za kiimani/dini yake uislam, akidai kuwa zinaenda kinyume na mafundisho ya dini yake na akajitoa kwenye safari ya maandalizi ya ligi, ambayo team yake inaendelea nayo huko Portugal akidai apewe jezi isiyokua na nembo ya hiyo kampuni.
Sasa hili la kwenda casino limemvulia heshima yake kama mwanasoka na kama muislam safi, kwa sababu huko kwenye macasino wote tunajua huwa kunakua na biashara gani, kama kamali, kubet, ma-stripers( wacheza uchi) n.k
Baadhi ya mashabiki wa Newcastle na wachambuzi wanadai Cisse alikua anajaribu kulazimishwa kuuzwa kwa club tajiri ambazo zimeonesha kumuhitaji hasa za Russia, na akatumia kigezo cha dini kama kisingizio ili aforce kuuzwa.
Kwa sababu wapo wachezaji waislam kwenye team ambao hawakua na tatizo na kuvaa hizo jezi, kina Ben Arfa, Sissoko na Tiote ila yeye akataka kudanganya watu kuwa ni muislam safi, sasa yatamtokea puani!