Je nifakati gani ambazo mtu wa PCB anaweza kusoma na akapata ajira kiulahisi
Kwanza tuanze na lugha sahihi. Wengi husema ni kozi gani mtu anataka kusoma. Kiswahili sahihi ni programu gani mtu anataka kusoma-kwani ndani ya program ndio kuna kozi tofauti ambazo lazima uzisome (core) na nyingine ambazo unachagua (electives) ili utimize matakwa ya programu upate digrii yako.
PCB ni tahasusi pana unaweza kusoma
1.
Program za afya (MD, D Dentistry, Pharmacy, Nursing na nyingine nyingi zilizo orodheshwa na TCU). Ugumu mkubwa ni kwa MD, DD, na B. Pharmacy nafasi ni chache hasa kama vyuo vilivyo zuiwa mwaka jana vitaendelea kuzuiwa kudahili. Unatakiwa point 8 za TCU yaani usinpungue P (D), C (C) na B (C) ushindani mkubwa hata hizo nane huna uhakika wa kupata. Nursing wanataka point 6.
2.
Program za Kilimo hizi cheki SUA ni program chache ambazo zina mahitaji mengine kama Agric. Economics na za Agric. Engineering karibu zote zilizobaki wanachukua PCB.
3.
Program za science education: Bachelor of Science with education
4.
Program za Science zinazohitaji ufaulu wa P au C au B, lakini nazo lazima ufaulu angalau principal mbili uwe na pint 4. Vyuo vyote vinavyo toa digree za science unaweza kupata. Mfano BSc Biology, BSc Chemistry, BSc Physics, BSc Zoology, etc.
5.
Program ambazo ni vigumu kufikiria: Kwa mfano IFM kijana wa PCB kachukulwa kusoma degrii ya ICT. Itabidi usome TCU Guide kwa umakini kuziona hizi.
URAHISI WA AJIRA LABDA YA KUANZISHA WEWE AU UWE NA SHANGAZI MWENYE AJIRA VINGINEVYO KOTE NI PATA POTEA. Mwaka wa jana wakenya walitangaza ajira za udakitari watu wakaogopa. Kuna kijana akaomba familia ikamshauri aachane na hiyo kitu, akasema akiitwa hatakwenda. Wakenya walipoweka ngumu (hawataki Dk kutoka Tanzania-unakumbuka walikuwa na mgomo), JIWE kuwaonyesha wakenya hana shida na kazi zao AKAWAAJIRI WALE WOTE WALIO OMBA KWENDA KENYA. Yule kijana akawaacha wenzake wanasugua bench. Hakuna formula. Hata programs zinazo pondwa watu hupata nafasi.