Fahamu Mfumo Mzima Global Position System ( GPS )

THE SPIRIT THINKER

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2019
Posts
419
Reaction score
654
GPS ni mfumo wezeshi ulioanzishwa kwa lengo la kupata urahisi wa ufanyaji Navigation ya eneo fulani la kitu fulani kilicholengwa na utambuzi wa muda uelekeo wa mahala fulani ambapo mtumiaji anaweza akaomba msaada wa utambuzi wa mahala fulani kutokea kwenye mfumo huu wa GPS

Mfumo huu ulianzishwa katika miaka ya 1978 na Jeshi la Nchini Marekani ambapo kwa wakati huo mfumo huu ulifahamika kwa Jina la Navstar GPS lengo kuu lilikuwa ni kupata usaidizi wa utambuzi wa eneo mahala husika la kitu kilicholengwa kutazamwa kama utambuzi wa vyombo vya usafiri wa majini na angani vifaa vya mawasiliano nakadhalika

Mfumo huu unatumia satellite maalumu ambazo zimepelekwa huko angani na kuwekwa katika maeneo yenye vipimo maalum ili kuweka uwiano sawa wa upatikanaji wa hudumu hii kwenye eneo zima la kuzunguka dunia yote

Satellites za GPS zinazunguka Dunia mara 2 kwa siku huku zikiwa katika Orbit ya pili ya Dunia zikiwa umbali wa km 20,180 kutokea usawa wa bahari mpaka sasa kuna jumla ya satellites 75 za mfumo huu wa GPS ambapo ni satellite 31 tu ndizo zipo kwenye operation mpaka sasa yaani zile zinazofanya kazi

Kikawaida mfumo huu unajumuisha segments 3 ili uweze kufanya kazi (i) space segment hapa ndipo eneo tunapoweza kuweka satellites zetu (ii) control segment hawa ndio watoa huduma yaani waongozaji wa mfumo mzima (iii) user segment yaani huyu ndiye yule.mtu wa mwisho mtumizi wa mfumo huu

Kumbuka kuna mambo 3 yanayofanyika kwa haraka zaidi pindi unapoomba usaidizi wa huduma hii
Utakaomba upatiwe msaada wa eneo gani ulilopo simu yako au kifaa chako kitatuma signal kwenda kwenye satellites halafu satellites zitapeleka ombi kwenye server zilizopo kwenye ground station ambapo wao kila muda huwa wana updates taarifa zao za mionekano mbalimbali ya uso wa dunia yetu pindi ground station watakapotoa ruhusa moja kwa moja satellite itafanya calculation ya eneo gani ulilopo na ndipo itatuma tena taarifa kwa ground station ili iweze kukuunganisha na ile visual picture ya muonekano wa eneo fulani la duniani huku satellite ikiwa inatembea moja kwa moja na wewe kokote utakapokuwepo

Kwa kuendelea ili uweze kupata huduma hii itabidi satellites zaidi ya tatu ziweze kuwa locked na wewe yaani satellites tatu ziweze kutambua kifaa chako mahali ulipo ili uweze kuendelea kupata huduma hii kokote utakapokuwepo duniani kote

Kwa uwepo wa satellites 31 inafanya mfumo huu kupatikana katika eneo zima la dunia kitaalamu tunaita Global service system

Kama utaona unapata huduma ya GPS kwenye kifaa chako tambua kuna mengi yamefanyika nyuma ya panzia .

Mwandishi : Moudy Swema Expert
 
Mkuu , ukitaka kuchora ramani au kicapculalte eneo kwa gps unafanyaje?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ