Fahamu kuhusu Android rooting....: case study.

ISO M.CodD

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
8,095
Reaction score
17,503
Rooting ni process ambayo inakupa super-user access kwenye device yako: namaanisha inakupa wewe na apps zako ruksa ya kudeal na hardware za simu directly na pia system directories za simu.
Kwa mfano, ukinunua simu kuna apps znazokuja ambazo kwa kweli huzihitaji, zinakula tu internal memory space na huwezi kuziuninstall. Kwa kuroot simu yako, utaweza kuinstall apps ambazo ztapewa hiyo super user access na kuweza kuzifuta hizo apps.
Faida za kuroot simu ni:

Kuremove deault apps (factory apps)

Kuinstall apps na kuziset kama system apps ili mtu asiweze kuziuninstall hata kwa factory reset. mfano anti-theft

Kucustomize simu yako mfano kubadilisha boot animation na boot audio (ile picha inayotokea wakat wa kuwasha na kuzima simu na sauti inayokuwa played)


Kucostomize various images na themes za simu yako

Kuweka efficient firewalls

Kufanya screenshot kwa kutumia apps kwa simu ambazo hazina built-in screenshot

Uses nyingine nyingi advanced kutegemeana na apps zako.

Jinsi ya kuroot simu.

Kuna njia nyingi sana za kuroot kutegeneana na android version ya simu, availability ya drivers za simu na uwezo binafsi wa mtu (Tech litteracy). Nakushauri ugoogle jinsi ya kuroot simu yako. Mfano kama unatumia HTC ONE, google "how to root HTC ONE".
Mimi ntaeleza njia niliyotumia. Nimeroot TECNO P3 na najua hii njia niliyotumia itawafaa watumiaji wa TECNO zote.
Kuna app inayoitwa POOT. Idownload kutoka play store. Then ukiifungua, itakuambia inataka Ministro II. We fuata tu masharti. Ikishamaliza kudownload wenziee, hakikisha kuwa USB debugging mode iko on (kwenye developer settings) umeiinstall kwenye phone memory, then fungua poot. Tap button ya press here to poot. Italeta mapichapicha ya kihindi lakini details zko hapa.... Baba 2023 |Android| Tech| Blogging Tips| Social Media| News: Root your Tecno P3, N3 and T3

Other options za kuroot:

Kutumia PC kupitia program kama super-one click.Ni simple, ila hii inahitaji device yako iwe na drivers au uzidownload kwahiyo kwa TECNO haifai sababu upataji wa drivers ni issue. Kwa wenzangu wa HTC na Samsung na kampuni nyingine kubwa, there you go.


Kutumia android apps nyingine kama z4 root na gingerbreak. Nyingi zinazingua. Zinaishia kustuck during the process, kutegemeana na device. Gingerbreak ni kwa ajili ya droid 2.3 Gingerbread. The best option ni kugoogle na kuona experts wameroot vipi.

Risks involved na rooting.
Warning: kama we ni mwoga, achana na hii kitu. Just settle with the basic.

Ukikosea steps in most rooting processes unaweza ukaua simu. Ujanja unahitajika.

Pia, baada ya kuroot simu, probability ya attack ya malware wanaoua system ni kubwa. Hivyo basi, ukishainstall app ya superuser,only grant root access to apps which you are sure of their uses. Unaweza kuua simu in no time!

Mengine uliza.
ISO, M.CodD
 
Ha hah ha h meipenda hii bt mmmh naogopa nisije nikaua ki-phantom changu buree
 
mkuu ISO.M.Cod vp kama nitaenda kwenye restore factory c ntakuwa nmeondoa takataka zote na cm kurejea upya
 

Ni elimu nzunri ya kitechnologia.
Ila kwa maelezo yako yotee yamehitimishi kua Risk ni Kubwa kuliko Return .

Na hakuna haja kuchezea shilingi chooni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…