Karata thanks a million but hapo nina maswali mengi sana juu ya hiki kitu manake reseach zilizopo hazituonyesh uhalisia na pia magonjwa yasiyokuwa na maambukizi yamekuwa kwa kasi ya ajabu. environmental pollution imechangia kwa kiasi kikubwasana plus environment toxicology na hapo ndipo penye shida sana manake kwa sasa hatujui tule nini kwa wakati gani na usalama wake uko wapi sas je nini kifanyike hasa kwa sisi tuloko huku dunia ya tatu, ukijumlisha kuwa lishe yetu ni mbaya na uwezo wa kifedha ni mdogo na mazingira yanayotuathiri siyo sisi tunao haribu bali hao walioko huko magharibi na pia mazingira ya kufanyia kazi ni mabaya?
pia sijui kama real you as heath practictioners huwa mnaongelea maswala ya occupational health manake jaman wafanyakazi wa viwandani are prone to cancerious and chemical pneumonitis at large. nimejaribu kutembelea viwanda baadhi achilia mbali safety gears but working environment siyo conducive kabisa, furans and dioxins plus pcbs zinaua watu.
Mkuu kwa kweli hali ni mbaya sana, Magonjwa yasiyoambukiza (Non communicable diseases) yameshika kasi kweli kweli, watu wengi sasa wanapoteza maisha kwa magonjwa haya (NCDs). Magonjwa ya moyo especially Hypertensive Heart diseases, Coronary arterial Diseases, Ischemic Cardiac disease kwa watu wazima na Congenital cardiac diseases kwa watoto yanaondoa watanzania kila kukicha. Magonjwa ya saratani nayo yameshika kasi, saratani ya kizazi na matiti kwa kina mama na saratani ya tezi dume kwa kina Baba wenye umri wa zaidi ya miaka 50 yameshika kasi. Ugonjwa wa kisukari na magonjwa yake pamoja na magonjwa ya figo (Renal failure) nayo ndo usiseme.
Serikali na donors wameelekeza nguvu zote kwenye magonjwa ya kuambukiza tu, kama vile HIV, TB na Malaria huku fedha zinazotengwa na Serikali na donor kila mwaka kupambana na magonjwa haya ni nyingi ukicompare na fedha zinazotegwa kupambana na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs). Serikali na Taasisi zake wala NGOs hazionyeshi kabisa nia ya dhati ya kupambana pamoja na kuaddress ukubwa wa magonjwa yasiyoambukiza nchini. Magonjwa haya sasa ni zaidi ya HIV maana NCDs yanaua haraka wakati HIV sasa umekuwa ugonjwa chronic ambao hauui haraka.
Magonjwa haya yamekuwa ni mzigo mkubwa kwa wananchi maskini maana matibabu yake ni ya gharama kubwa sana, zamani tulikuwa tunayaita "magonjwa ya matajiri" kwa mfano, matibabu ya saratani ni ghali sana (gharama za Chemotherapy zinaweza kufikia USD 10000 kwa mzunguko mmoja wa chemotherapy), Gharama ya matibabu ya saratani za damu (Bone marrow transplant ) yanafikia USD 35000 mpaka USD 40000. Kwahiyo, watu maskini wasiokuwa na uwezo wanapoteza maisha kila kukicha.
Ni kweli katika nchi yetu hatuna data (research) iliyofanyika kuonyesha magnitude/ukubwa wa tatizo nchini, lakini unaweza kufanya utafiti mdogo kwa kwenda japo siku moja katika hospitali ya Saratani Ocean road ili ukajionee ungezeko kubwa la wagonjwa wa saratani.
Nini kifanyike?
Kwa mtazamo wangu napenda kushauri mambo yafuatayo:
1.
SERA- Kuwe na Sera mahususi kuhusu NCDs ambayo itakuwa DIRA itakayotuongoza katika vita dhidi ya NCDs, sera ambayo itaweka bayanamasuala mbali mbali katika harakati za Taifa kupambana na kudhibiti NCDs, mfano, ushirikizwaji wa Sekta zote katika vita dhidi ya NCDs
2.
ELIMU- Elimu ndo msingi katika mapambano ya kuthibiti NCDs, Serikali na Taasisi sizizo za Serikali zitoe Elimu kwa umma kuhusu NCDs. Hii itacreat awareness katika jamii kwa ujumla na kufanya wananchi wengi wayatambue magonjwa haya na jinsi ya kujikinga nayo (preventive is better than cure). Elimu ianze kutolewa kuanzia kwenye ngazi ya shule za msingi.
3.
MSUKUMO WA KISIASA NA KISERIKALI NA UONGOZI- Kunatakiwa kuwepo na msukumo na dhamira ya kweli kunakoambatana na vitendo kutoka Serikalini na wanasiasa ili kuongeza vita dhidi ya NCDs. Ni muhimu pia uwajibikaji kisiasa na Kiserikali katika vita dhidi ya NCDs uimarishwe katika ngazi zote.
4. Nitaendelea siku nyingine………