Ndugu Masanja,
Unaifahamu vizuri maana ya neno "double standards". Neno hilo kwa kiswahili sijui ni lipi, ila nadhani halipo. Kuwa na neno la kitu fulani ina maanisha kuwa kuwa hicho kitu ni "common" hapo mahala! Hivyo basi, neno double standard kuwepo kwenye lugha yao inaonesha kuwa ni jambo la kawaida kabisa kwao. Hao jamaa kwa double standard ndo wenyewe.
Ingekuwa Africa ina viongozi wenywe vichwa (yaani wenye akili timamu) hapo hapo ndo nasisi tungelamba bingo! Yaani wangeongea vizuri na Muammar halafu wamshawishi alipe hiyo fidia (ikiwezekana hata nchi tofauti zikaichangia Libya kwa pesa kama fidia hiyo ni kubwa sana).
Baadaye miezi/mwaka hivi nasi tunaanza kudai fidia kibao kwa vitu ambavyo ulaya wametuuzia na vikatuua au kutudhuru! Kwa Tz tunaanza tu kiulaini na yale mabomu ya Mbagala, tunaingia kwenye silaha walizomuuzia Idi Amin halafu akatuvamia, tunaenda kwenye kile kivuko nyanya kilichokuwa kinaua watu kila siku kigamboni kilichokuwa kimenunuliwa toka UK, halafu tunaenda MV Bukoba (nayo ilikuwa nyanya-na wao walikuwa wanafahamu). Halafu tunaanza kudai fidia ya zile kemikali chafu wanazotupa (dump) afrika kila leo. waTz tukianza ishu ya radar, ndege ya raisi na narushwa ilotembea basi itabidi watugee bure tu hiyo Radar. Fidia ya watumwa, madini, maliasili na vingi vya kale tunavicha ili tuanze na cha mtoto (yaani vitu vidogo vidogo kwanza kama mabomu Mbagala nk). Halafu tunawarudia tena na sigara zenye sumu kali wanazotengeneza kuzileta kwetu kuuza (ingawa viwanda ni vivyo hivyo, sigara za kupeleka Afrika na Asia huwa zinatengenezwa na sumu kali zaidi na pia zinakuwa na addiction rate kubwa zaidi)
Infact, mimi niliposikia hivyo nilicheka na kusema kuwa ama kweli duniani kuna mambo na akutukanaye hakuchagulii tusi! Nikajisemea hawa jamaa kweli wanatuona sisi mbumbumbu! Kwani tukianza kudaina fidia sidhani kama kutakuwa na haja ya waTz na wa afrika engi kufanya kazi tena.