Eti mwanaume ni malighafi....!

Nanoli

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
3,739
Reaction score
5,979
Eti wanaume ni Malighafi!

Jamani....

Nikiwa safari kuelekea Nairobi nilifanikiwa kuonana na mama mmoja Mchaga aliyefanikiwa sana. Ana hoteli Arusha, Moshi na pia ana export kahawa.

Nilijiuliza sana huyu mama amewezaje?
Ikabidi nianze kumchimba.

Aliponiambia wanaume ni Malighafi, nilishtuka sana. Nikaomba anidadavulie ....

G: Unasemaje ? Wanaume ni malighafi? Sikuelewi? Una maana gani?

M: Usinielewe vibaya, kwanza inabidi ujue maana ya malighafi. Nadhani unajua malighafi ni nini. Malighafi ni bidhaa inayohitaji kuongezewa thamani ili upate faida zaidi. Au unahitaji kuisindika kabisa ili iwe na thamani kwa faida yako.
Mimi kama mwanamke kwangu mwanaume ni malighafi inayotakiwa kuongezewa thamani kwa faida yangu.

G: Sijakuelewa kabisa mama.

M: Sisi wanawake tuna nguvu isiyo kawaida. Mungu akikupa mwanaume, ni kama malighafi ...unatakiwa kuongeza thamani, kumtengeneza unavyotaka kisha unamtumia kuwa unavyotaka. Mwanamke anaweza kumwamsha mwanaume aliyelala na kumfanya kuwa Rais, au mwanamuziki mkubwa halafu anaweza kumtumia kuwa anavyotaka. Wanawake wa siku hizi, wakipewa mwanaume wanataka awe amekamilika yaani finished product ili wamtumie. Huo ni ujinga. Wanawake tumeumbwa kuhamasisha. Tumeumbwa kumpandisha mwanaume. Mwanaume ni kichwa lakini kwenye familia mwanamke ni moyo.

G: Bado sijakupata kabisa.

M: Ngoja nikupe mfano. Mume wangu mimi alikuwa mwanafunzi wa chuo nilipokutana naye, mlevi na asiyejielewa kabisa. Lakini kuna kitu cha tofauti nilichogundua...alikuwa na akili. Kwangu ilikuwa ni malighafi yenye utajiri. Nikapiga mahesabu yangu, nikaingia kwenye mahusiano. Nikampa anachokitaka akapagawa. Kisha nikashika usukani. Nikatafuta njia akaacha pombe, akawa msomaji sana mpaka akafaulu chuo kikuu. Amemaliza uinjinia, nikampelekesha akanioa. Ninamjua wapi pa kumgusa. Alipomaliza chuo, nikamwambia sitaki awe mwajiriwa akagoma. Uoga. Nikamwacha, mshahara ulipoanza kuingia nilishika mimi .... Nikimpa anatumia pombe. Nikaanza kuchukua akiba yeye bila kujua, nikanunua mashamba, viwanja, nikaanzisha mgahawa. Nikamwita kama mgeni rasmi kuja kuzindua. Nikampeleka kwenye mashamba niliyonunua. Akapagawa. Nikahamisha akili yake yote, kwangu.
Tukaanza kushirikiana pamoja mpaka tukasimamisha hoteli. Mume wangu alikuwa hapendi biashara lakini baada ya kumbadili akapenda biashara kunizidi. Unajua nini kilitokea. Aliacha kazi na kuweka nguvu kwenye hoteli ndogo, tukafanikiwa mpaka hoteli kubwa ikajengwa.

Mashamba zaidi yakanunuliwa. Watoto wetu wanasimamia biashara zetu. Mume wangu ni mpambanaji hatari kwasasa. Unajua kwanini? Kwangu alikuwa ni malighafi, nikaamua kuongeza thamani.

G: Aisee!! Eeh?

M:Wanawake wa siku hizi wanatafuta wanaume walioongezewa thamani, ili wawatumie. Ukiona mwanaume yupo juu fahamu kuna starring nyuma ya pazia aliyesababisha. Mwishoni wanatumika wao kama vyombo vya kujistarehesha na kutupwa. Mwanamke unatakiwa kuwa na akili mara nne ya mwanaume, na usijivune kama una akili. Ukikuta mwanaume ana akili na unajua unaweza kumtengeneza chukua na ongeza thamani.

Ukichukua kilichoongezwa utapigwa tu. Utaachwa.

Mfano kama mimi mchaga nikiolewa na mwanaume ndani ya miaka mitano hamjajenga, asihukumiwe mwanaume. Mwanamke ndiyo kimeo.

Mwanamke ni msababishaji, uliza matajiri wakubwa duniani. Uliza watu wakubwa maarufu, uliza akina Napoleon, uliza akina Obama, uliza akina Albert, uliza utajua....nyuma yao kuna nguvu inayosababisha mambo makubwa.

[emoji124][emoji124][emoji124]USIPOELEWA MWAMBIE MUHUDUMU AONGEZE GLASS .

"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
 
Hivi ukielewa ndio huruhusiwi kuongeza glass???

Mkono naunga hoja
 
Mkuu kwa ulivyo kaza kichwa umefanya wote tuelewe huku si kwa mchanganuo huo.
 
Ndio mwanaume ni malighafi wakati mwanamke ni bidhaa
 
Wanawake wote mkiwa kama huyu wote mtaolewa: Yeye kwake mwanaume ni malighafi

Naomba niishie hapo....
[emoji124] [emoji124]
 
Wanasema "Never marry for potential". Unaweza ukaolewa na mtu mlevi halafu uchakarike kumtengeneza mwishowe ukakuta kumbe ni mlevi tu then you are stuck forever.

Bora nichakarike mwenyewe hayo manguvu yote nitumie mimi kujiinua halafu nikutane na mwanamme ambae tumelingana level. Umetoa mfano wa Barack Obama na Michelle; wale wote wamesoma vyuo vya Ivy League ( Harvard, Princeton), na si kwamba Michelle alimkuta anauza burger mahali akamsimamia mpaka akafika kuwa raisi. Wote wawili walikuwa na akili na maarifa.

Nakubaliana kuangalia potential ya mtu, lakini isiwe kazi yako kumsimamia kila kitu, kumnyanyua n.k. Wewe atakunyanyua nani muda wako ukifika? ndo wale unawanyanyulia hoteli wanaalika vimada kuja kulala wewe unasimamia viwanja na watoto nyumbani😀

Enewei, ni ushauri mzuri kumpa moyo mwanaume, lakini angalia usije invest kwenye gari bovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…