Eti hili nalo kosa

iMind

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,232
Reaction score
5,534
Duu ndoa hizi bwana. Leo nimewahi kurudi home saa 11 jioni. Wife alikuwa ameaga kuwa atachelewa kurudi na siku zote huwa anarudi kabla yangu. Mimi narudi saa 2 hadi 4.

Sasa kuwahi kwangu kurudi anahisi eti nilikuwa nammendea house girl. Yaani yuko njiani anarudi anasema leo tuta mkoma.

Ukweli ni kwamba sijawahi kuwa na hata mawazo ya kutembea na huyo hg. Na mimi niliwahi kurudi kwa kuwa yeye alisema atachelewa kurudi nikaamua niwahi kucheza na watoto ili wasije wakawa wapweke jioni ikiingia. Dah noma sana
 
Hizi ndoa bwana?

Amekurupuka tu ama umeshawahi kumpa nafasi ya kuhisi wewe sio mwaminifu kwake?
 
He he he he, kuna kkitu hujasema sawa.
 
Mmmmmmmh

Sidhani kama kuwahi ndo sababu ya kukuhisi hivyo
 
Lakini kama alikuwa anataka kukumata ugoni ndo angekwambia kweli anatania tu huyo.
 
Ulishawahi kumfanyia tukio siku za nyuma na bado hajasahau
 
kwa hiyo wewe ni marufuku kurudi home kabla wife hajarudi? duh!
 
Sijawahi kufanya tukio na hg wala kuonyesha dalili zozote. Ila huyu house girl wa sasa alikuwa kwa dada yake. Nasikia kwamba dada yake alimtimua baada ya kuhisi kuwa ana ukaribu na mumewe. Mume wa huyu dada ni mtu asiye jiheshimu na asiye mheshimu mke wake. Hivyo siwezi kubisha hata kidogo kwamba hawezi kumtaka hg.

Hg huyu ni binti mdogo na mrembo. Ingawa mke wangu hakuniambia hiyo story ya dada yake kwani niliambiwa na house boy wa dada yake. Ila toka aingie hapa ndani mke wangu amekuwa very consious. Yaani ni ugumu wa kupata hg tu ndo umemuweka huyu dada hadi leo.

Wiki 3 zilizopita ali niambie eti anahisi huyu house girl anatembea na mdogo wangu ambaye anaishi hapa kwetu. Akataka niwakanye. Nikamwambia mimi siwezi kuwakanya kama sina ushahidi. Na yeye hakuwa na ushahidi wa maana. Ila uchunguzi wangu binafsi hauonyeshi dalili zizite za kuwa wanauhusiano.

Sasa leo na mimi nimetuhumiwa. Huyu dada hi hg mzuri na anafanya kazi vizuri sana. Mimi mara nyingi sikai nyumbani na wakati wote ninaokuwa nyumbani mke wangu anakuwepo. Leo ndo imetokea hivyo.
 
Hop keshafika tuambie pamechimbikaje Leo hapo?
 
Inwezekana mienendo yako kaisha ishtukia haswa mnapo jadili utendaji kazi wa msaidizi huyo wa kazi, labda kuna vitu huwa anakutega wewe unamtetea kwani wanawake ni very smart katika mambo ya mapenzi ya ndoa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…