Na mimi nimeshangaa ujue. Labda kama huyo rafiki alimnunulia hizo shanga akamuwekea kitu kibaya. Ukute mke alitaka kuongeza chachandu kwenye mahaba jamani.
Kuhusu marafiki, inabidi mtu binafsi apime aina za marafiki alionao. Sio kwamba tu HS ntaolewa afu nikatishe urafiki na rafiki zangu kisa wao hawajaolewa mmh. Sio kila ambaye hajaolewa ni mbaya au atakushauri vibaya. Unawajua rafiki zako wazuri na wabaya, wale wabaya punguza urafiki nao na usiwaelezee mambo yako ya ndoa. Afu at the end of the day wewe ndo muamuzi wa mwisho, ushauri utapewa hata na aliyeolewa mwenzako ila akili kumkichwa.