Habarini wanazuoni na wabobezi wa elimu.
Niko mbele yenu kuna masuala nataka niyajue juu ya taaluma ya OUT (open university of tanzania). Kwa watu waliosoma au kuwa na uelewa juu ya hii system ya kupiga shule..
1. Inakuaje kuaje (maana naona ni ngumu sana kuifaulu vilivyo kutokana na maneno ninayoyasikia kua kila kitu unasoma mwenyewe na paper zake ni ngumu sana)
2. Kuna ku supp/carry/disco?
3. Unaweza ukatoka katka hiko chuo ukawa vzr kiasi kwamba ukaaminika safi kuliko hii taaluma ya vyuo vingine.
4. Nilipokua chuoni enzi hizo pale ud nilisoma kimagumashi na nilipofika mwaka wa mwisho nilikua nimechoka sana. Sasa nawaza kwa open ya kujisomea mwenyewe itakua ni changamoto hivi kuimudu.
5. Mimi nimepata masters scholarship ktk chuo fulani hapa nchni je nitaweza kum udu na hii ya open university? Maana nataka nisome masters mbili kwa wakati mmoja.
6. Shule ya OUT inaleta mood katika kusoma au ni ngumu sana?
Nawasilisha naombeni msaada, na pia mimi nataka nisome masters level.