Dunia yamgeuka kagame...

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,847

Jarida maarufu Uingereza lamwita Bwana wa Vita

TASWIRA ya kimataifa ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye katika siku za hivi karibuni aliibua mzozo wa kidiplomasia na Rais Jakaya Kikwete, inaonekana kuchukua mwelekeo wa kuchuja badala ya kustawi kwa namna ilivyokuwa miaka michache tu iliyopita, MTANZANIA Jumapili limebaini.

Baada ya kuvuma kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, Kagame, aliyekuwa akibeba taswira ya mtu shupavu na shujaa, amegeuka na kuanza kuonekana kiongozi mpenda vita, makuu na rais anayeweza kusababisha kuibuka na kukua kwa ufa mkubwa wa kimahusiano kati yake binafsi na viongozi wenzake wa ukanda huu wa Afrika.


Nje ya bara hili, kuzorota kwa taswira ya kiongozi huyo kunaonekana kuanza kugusa hisia za wachambuzi wa masuala ya kisiasa, wanadiplomasia wanaoheshimika na viongozi wakuu wa mataifa ya Ulaya, Marekani na ndani ya Umoja wa Mataifa.

Siku chache baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama, kukaririwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani akimtaka Rais Kagame kuacha kukisaidia kijeshi kikundi cha waasi wa M23, kidole hicho cha lawama kinaonekana kuungwa mkono kwa kasi na makundi mengine ya kimataifa.

Kagame, ambaye kwa miaka mingi amekuwa kiongozi kipenzi cha mataifa ya Ulaya na hasa Marekani tangu alipofanikiwa kumaliza mapigano yaliyosababisha mauaji ya halaiki nchini kwake mwaka 1994, katika siku za hivi karibuni taswira yake inaonekana kubadilika na kuchukua mwelekeo wa lawama zaidi kuliko sifa.

Matamko na maandishi yenye mwelekeo wa lawama ambayo yalitolewa dhidi yake katika siku za hivi karibuni yameanza kuchukua mwelekeo unaoonyesha kwamba Kagame wa sasa si yule tena aliyekuwa akitajwa kuwa mfano wa kuigwa wa viongozi wapenda maendeleo na wazalendo wa kweli katika Afrika.

Tukio la hivi karibuni kabisa, ni makala ya uchambuzi iliyochapishwa katika gazeti la Uingereza la The Telegraph, ambayo ilieleza namna majeshi ya Rwanda yalivyokuwa yakijipenyeza ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kutoa misaada ya silaha na vyakula kwa kundi la waasi wa M23, ambalo limekuwa likipigana Mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 2010.

The Telegraph katika makala yake hiyo lilidurusu ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch, iliyotolewa mwezi mmoja uliopita, ambayo pamoja na mambo mengine, iliainisha ushahidi wa namna vikosi vya Jeshi la Rwanda vilivyokuwa vikishiriki katika vitendo vya kiharamia ndani ya DRC.

Katika uchambuzi wa ripoti hiyo, The Telegraph limeainisha kwamba ndani ya Rwanda, wanaume na vijana wadogo wenye umri wa miaka 15 wamekuwa wakilazimishwa kupewa mafunzo ya kupigana kijeshi kwa lengo la kulinda maeneo yenye utajiri wa madini katika mpaka wa nchi hizo mbili.

The Telegraph limeandika kuwa licha ya utetezi wa awali wa Uingereza juu ya misaada inayopelekwa Rwanda kuwa haimaanishi nchi hiyo inakwenda vitani Kongo, lakini sasa uhalisia wa tuhuma dhidi Rwanda umejiweka hadharani.

Andrew Mitchell, Katibu wa zamani wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza, alikuwa mstari wa mbele wa kumtetea Rais Kagame dhidi ya shutuma za kuchochea mapigano Kongo, pamoja na kupingwa vikali na mbunge wa nchi hiyo, lakini Julai mwaka jana alifanikiwa kuidhinisha msaada wa pauni milioni 16 kwa ajili ya serikali ya Rwanda.

Awali Mitchell alipata kumshawishi Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, kwamba madai yaliyokuwa yakiihusisha serikali ya Kagame na tuhuma za kuwaunga mkono waasi wa M23 hayakuwa na ukweli.

Ushawishi huo ambao ulipingwa vikali na wabunge wa nchi hiyo katika mjadala wa bajeti ya misaada, hatimaye ilisababisha Mitchell alazimike kung’atuka katika nafasi hiyo ya uongozi kwa sababu za kisera.

Kitendo cha wabunge kupinga mtazamo huo wa Mitchell kutokana na kuwa na imani yao kwamba Rwanda imekuwa ikisaidia kundi la waasi wa M23, mrithi wa kiti chake, Justice Greening, alilazimika kufuta misaada ya kifedha kwa taifa hilo yenye thamani ya jumla ya pauni milioni 21 mwishoni mwa Novemba, mwaka jana.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Kagame alipata kukaririwa akieleza namna alivyokuwa akikerwa na maamuzi ya Jumuiya ya Kimataifa kuikatia misaada Rwanda, hatua alizozielezea kwamba zitalifanya taifa hilo liendelee kustawi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ziliibuka tuhuma zilizoelekezwa kwa Kagame na Majeshi ya Rwanda kwa namna walivyokuwa wakishiriki katika mapigano ndani ya DRC.

Alikuwa ni Balozi wa Kudumu wa Ufaransa ndani ya baraza hilo, Alexis Lameck, ambaye alikariri taarifa za kutoka kwa Msemaji wa UN aliyeko Kinshasa nchini Kongo, Edmond Mulet, ambazo zilikuwa zikiinyooshea Rwanda kidole cha namna ilivyokuwa ikishirikiana na M23.

Shutuma mpya dhidi ya Kagame zinakuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja sasa, tangu gazeti hili la MTANZANIA Jumapili lilipoandika kwa mara ya kwanza namna taswira ya sasa ya kiongozi huyo inavyoweza kuwa mwanzo wa hatma mbaya kwake.

Katika gazeti hilo, ilielezwa namna Kagame anavyokabiliwa na hatari ya kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kama ilivyopata kuwa kwa aliyekuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor.

Kama ilivyo kwa Kagame anavyohusishwa na vita ya Kongo, Taylor alituhumiwa kwa miaka mingi kama mbabe wa vita vya Sierra Leone, ambayo iligharimu maisha ya takribani zaidi ya watu 50,000.

Kwa sasa Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela, baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone.


SOURCE:Mtanzania
 
Inatia uchungu sana kuona kila siku tunaongelea 'RISE AND FALL' ya viongozi wa Africa! Kwa nini viongozi wetu hawajifunzi kutokana na misemo rahisi ya kimila mfano 'MGEMA AKISIFIWA, TEMBO HULITIA MAJI?' Viongozi wetu wanajifunza na kujua wazi kwamba 'POWER CORRUPTS, AND ABSOLUTE POWER CORRUPTS ABSOLUTELY' lakini hawatumii elimu hii kujipima kwa vitendo na mwisho wake wanaishia kwenye majanga!

IT'S NOT TOO LATE FOR KAGAME, HE CAN STILL DO A LOT TO SAVE HIMSELF AND RWANDA IF ONLY HE CAN SWALLOW A LITTLE BIT OF HIS PERSONAL AND HIS NATION'S PRIDE!
 
Kagame is ending up so soon and he will end up terribly, it's a matter of time.
 
Tatizo la viongozi wa kiafrika ni kwamba wanacho fikiria na kuitetea ni maslahi yao wenyewe kwanza badala ya kuitetea nchi na wananchi wao. Tuseme ni sisi waafrika wote hata kama tutasoma vipi na kuona wenzetu walivyo endelea bado akili zetu ziko nyuma sana. Karibia kila nchi ya kiafika Ina waasi na hao waasi wana sababu zao. Kuna waasi waliochoka na vitendo vya viongozi wa nchi kwa mfano madictators. Na kuna waasi wanao shinikizwa na matajiri toka nchi za kitajiri.kama mmeona film ya DiCaprio. Inayo itwa Blood Diamond. Sasa mtu unajiuliza kwanini sisi tu Afrika au developing countries??? Rwanda imepandisha ushuru wa lory toka tanzania sasa je anamkomoa nani kama si wanainchi???
 

Kweli mangi wangu Brown73 Anawakomoa wananchi wake na kumpandisha chati kigeugeu Kenyata! Lakini daima tukumbuke kwamba 'MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA!'
 
Last edited by a moderator:
Bado anaweza kujirekebisha! Anayo nafasi ya kuweka mambo yake sawa, japo sidhani kama mtazamo huo anao.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Rejea tamko la Membe hivi karibuni:wameshaongea kwa siri JK na PK...
 
Nafikiri wazungu hawana rafiki wa kidumu ila maslahi (permanent interests not permanent friends). Kagame amekuwa rafiki yao na sasa wamegeuza kibao.
Kumbukeni jinsi walivyomsaidia Mubarak wa Misri, Mobutu, Osama, nk. Leo wako wapi?
Tunatakiwa kuwa makini. Kesho inaweza kuwa zamu ya viongozi wa nchi kama Tanzania nk.
Je wao wanaotaka kuishambulia Syria, Iran, North Korea, nk ni wasafi kiasi gani? Wameziacha wapi nchi za Afganistan na Iraq? Wao ni wa kuchambua wengine?

Mimi nahisi kila nchi au uongozi hapa duniani una matatizo yake.

Nakumbuka Rais Mugabe arivyo wafanya marais wenzake wakae kimya kwenye mkutano wa AU pale walipokuwa wanataka kumwonyesha kuwa anaongoza kwa mabavu miaka kama mitano na nusu iliyopita? Aliwaeleza wakae kimya na kusema aliye safi na aeleze ili naye aonyeshe makosa yake.

Tuangalie nchi iliyo na amani tangu kupata uhuru. Je nchi yetu, viongozi wako salama? Vipi rushwa? Vipi kuhusu kunyanyasa raia wake wanaoleta kujua? Au tomesahau jinsi wanavyong'oa kucha na meno na macho nk?! Tumesahau ya mwandishi Mwangosi, kuuawa bila ya kupata haki ya kisheria mpaka sasa?! Ingawa siamini kama suluhu ni kuandamana kwa waliokufa Mtwara; je walitakiwa kufa pamoja na kwa kutokuwa na silaha?

Tumeshasahau yaliyotokea Mwembechai miaka ya 1990 na Zanzibar 2001? Kulikuwa na umuhimu wa watu kuuawa au wangetakiwa waishi na serikali itatue kero walizokuwa nazo?

My take
Nchi zote na viongozi wake waanzie makwao kabla hawajanyooshea wenzao kidole; maana vidole vingi vinaonyesha kwao.

Anjo
 
Kagame siku zake zinahesabika maana matumizi yake tayari hayahitajiki tena na nchi za magharibi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…