Tumeamua kabisa ku dramatise na maisha yetu kama taifa. Tukisahau kabisa vipaumbele vyetu na changamoto zetu.... Tukisisimuliwa na matukio yasiyo na tija ya wakosa maono, wakosa tafakuri huku umbea na upuuzi mwingi vikipewa nafasi kubwa kwenye bulangata za wengi
Ni dunia za Instagram na ulingo wa siasa... Zikiishi kwenye ulimwengu wa Jamiiforums kama mshindo nyuma....
Vinatokea vibweka huko kwenye siasa, watu wazima wanatamba na kuoneshana uwezo wa kuongea na kupayuka vitu vya kufikirika, vingine vikiwa ni upuuzi mtupu... Vitu hivyo haviandikwi kwenye vyombo vingine vya habari unavikuta JF
Watu wazima wanashadadia na kujadili mambo ya watu binafsi kutwa kucha kila mtu akionyesha umahiri mkubwa kwenye ushukununu na umbea.... Mambo ya Instagram.... Mshindo nyuma ukiwa JF
Ni Jamiiforums pekee ikisaidiwa kwa karibu na makundi ya wasapu ndio inakuwa kiunganishi cha hizo dunia mbili... Hakuna magazeti tena, hakuna radio tena, hakuna luninga tena.... Ni ulimwengu wa JF ndio kimbilio la mrejesho na yanayojiri....
Je hili linatokea kwa bahati mbaya ama kuna ma engineers nyuma yake? Kwa faida ya nani? Ili iweje? Taarifa za kuunga mkono juhudi sio habari tena... Sasa mijadala ni habari za mahusiano ya watu mikwaruzano na umbea wote.... Viongozi wapayukaji nk
Ni dunia mbili ndani ya ulimwengu mmoja... Lakini hazina maana wala manufaa kabisa kwa mustakabali na ustawi wa taifa!
Pengine kuna dunia nyingine zipo ila hatuzioni ama zimefichwa!?
Wako wapi wanazuoni wetu? Wanagenzi? Wasomi wetu? Wachambuzi wetu? Hawaonekani...!
Twendeni tukapate nguvutumbo