Mungu yupo na ndie alieumba ulimwengu na vilivyomo kwa ustadi usioweza kumithilika.
Hakuna chance inayoweza kutengeza mifumo ya maumbile mbalimbali iliyopo ulimwenguni kwa ustadi ambao akili zetu huishia kustaajabu na kujiuliza ni kivipi kuna umbile kama hili na kwa nini lipo.
Ufinyu wa ufahamu wetu umetufanya kila leo wanasayansi kubadili kauli juu ya sayari na mifumo yake. Na bado hata kwa elimu hii ndogo tunayofunguliwa hatutaweza kuyamkini na ku comprehend kila jambo la Muumba.
Mwenyezi Mungu ametupa akili na Free will / freedom of choice katika kuyaendea yale ambayo ameyaamrisha na kuyaumba. Ni katika uhuru huo wapo watakaopinga uwepo wa Mungu na kuyapinga Maandiko yake kwa kuwa tu akili zao zinaona kuna contradictions. What if hizo contradictions zina exists katika akili zao tu kwa kuwa wameamua kuchagua kujifunga kuelewa yale ya Mungu Muumba?
Leo watu wanasema kwa nini aumbwe shetani kama kweli Mungu ni All Loving, the most merciful. Je shetani aliumbwa Shetani au kwa uamuzi wake alichagua kuwa shetani na kukataa misingi ya haki aliyoumbiwa? Tunaambiwa kwa miaka Dahr Iblees alikuwa ni katika kundi la waabudio waliokuwepo mbinguni, lakini kwa jeuri, inda, kiburi na inadi aliacha kufuata ktk misingi ya haki na kuchagua njia ya udhalimu.
Kuna njia kuu mbili za kufuata, moja ya kuamini na njia ya kukufuru. Uhuru ni wako kuchagua yale aliyochagua iblees na kukataa ya Mungu. Hivyo ndivyo utakavyochagua outcome ya maisha yako baada ya kifo.
Huyo ndie Mungu alieumba kila kitu, cheupe vs cheusi, kizuri vs kibaya, imani vs kufuru, pepo vs moto, +vs -, mume na mke na variations zote zilizopo ili apate kututahini (LICHA ya kuwa anajua outcome ya mtihani) nani kati yetu ni mbora katika kuyafanya mema.
Ushauri kwa wanaobishana kuhusu Dini, Tukae chini tuzisome dini zetu. Tumfahamu Mungu ukweli wa kumfahamu ili tuweze kunuabudu ipasavyo na kujua hekima yake katika kila alichokiumba.