Dunia bila vita/machafuko haiwezekani?

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
16,500
Reaction score
38,406
Toka nimeanza kupata ufahamu (early 90's) ni mengi nimeyasikia kuhusu machafuko ndani ya nchi mbalimbali, vita baina ya nchi na nchi mpaka kile kichohubiriwa kama ugaidi na vita dhidi ya ugaidi.

Orodha ni ndefu kuanzia

1. Vita ya Ghuba

2. Vita vya kiraia (Croatia, Afghanstan, Liberia, Congo, Yemen, Bosnia, Rwanda, Burundi)

3. Vita ya mipaka (India na Bangladesh, Ossertia ya kusini na kaskazini)

4. Vita kati ya serikali na waasi (Uganda, Sirlanka, Russia/Chechniya)

5. Vikundi/ mashambulio ya kigaidi (Alqaida, Boko haram, Alshabab,ISIS, Fatah, Hamas, Ezborah)

6. Mashambulio ya US na washirika wake dhidi ya mataifa mengine (Cosovo, Iraq, Afghanstan, Libya)

7. Russia dhidi ya Georgia

Na mpaka siku za hivi karibuni habari zinazogonga vichwa vya habari ni ugaidi na mapigano ya hapa na pale, Alshabab bado wanaendeleza mashambulio, Syria bado hakueleweki, North Korea bado wanaendelea kuwa kitisho dhidi ya ulimwengu wa magharibi.

Ninachojaribu kujiuliza...

1. Hivi haiwezekani hizi vita na migogoro ikakoma na kufanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi?

2. Je dini zimefanya migogoro kuongezeka ama inasaidia kuipunguza? Maana vita/migogoro mingi lazima dini/imani vitahusika kwa namna moja au nyingine.
 
Daaah mkuu yaani hii mikasa sijui itakwisha lini atleast tuwe na amani
 

Attachments

  • bitmoji-20170705115205.png
    11.5 KB · Views: 28
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…