Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
Mh! I doubt this, what about, Stan Katabalo, Gilman Rutihinda, Steven Kibona, Horace Kolimba, Imrani Kombe, Edward Sokoine, Koplo Rashid Lema e.t.c.
Inasemekana imran kombe alishugulikiwa na mzee mwenyewe baada ya wakuu wa intelejentia kumweleza anavujisha siri za serekali ya ccm kwa mzee wa kiraracha, ndiyo mana mzee wa kiraracha alikua kila kukicha anawalipua
Hata hawa nao walisema CCM imepoteza muelekeo? Mmoja alikuwa anaandikia gazeti la mfanyakazi, mwingine akawa gavana wa fedha na mwingine waziri wa fedha, huyu nae akasababisha mtu azikatae pesa zake zikiwa ndani ya gunia.......aah huyu si alikuwepo wakati mwenzake anamwelekeza kwa simu kuwa wawaue wote wasimwache hata dereva taxi!Mh! I doubt this, what about, Stan Katabalo, Gilman Rutihinda, Steven Kibona, Imrani Kombe, Edward Sokoine, Koplo Rashid Lema e.t.c.
Wimbi la mparanganyiko wa ccm linazidi kushika kasi kila kukicha,baada ya mtoto wa mkulima kuwataka viongozi wastaafu kutumia vikao kueleza mawazo yao.Agizo hilo limepuuziwa baada ya mmoja wa viongozi wastaafu Dr Hans Kitine kukiponda wazi wazi chama hicho.Akiongea ktk kipindi kinachorushwa na Channel ten cha Je tutafika? Kitine amesema kuwa ccm IMEPOTEZA MWELEKEO maneno yaliowahi kumgharimu aliewahi kuwa katibu mkuu wa ccm wakati huo marehemu Horace Kolimba.Swali langu kwa great thinkers je Dr kitine atasalimika kweli kwa hiyo kauli? maana ukweli unauma!
inategemea ukweli gani,chama kilichokomaa kisiasa hakitakiwi kuteteleka kwa statement za watu kama kitine.swala la kuangaliwa ni je chama hicho kinafanikiwa kupata na kutimiza malengo yake?mfano kushinda uchaguzi,idadi ya wabunge wengi nk halafu ndipo utakapojua mwelekeo wa chama.kifo cha kolimba ni ccm au mungu?na kitine siku zake zikifika ataenda mbele za haki kama wengine wote binadamu itakavyokuwa.
Kama kawiva alishindwa vipi kucoverup scandal yake hadi wakamlipua mnasifia mijitu kishabiki.ama mlikua bado kindergaten hamjui alifanyaga nini
Hata mie nilitazama kipindi hicho jana cha channel ten.Dr Kitine ameweka wazi na kwa mifano halisi udhaifu uliopo ndani ya CCM.Moja ya kitu alichotanabaisha ni pale aliposema kuwa baadhi ya viongozi waliopo na wastaafu wameamua kuongea nje ya vikao kwa sababu siku za hivi karibuni vikao hivyo vya CCM vimekuwa havina agenda za maana, na badala yake vimegeuka kuwa ni ulingo wa kukejeri wenye mawazo tofauti, fitina, kushambuliana miongoni mwa makundi yanayosigana ndani ya chama.Kutokana na hali hiyo watu wenye akili zao wanaona ni bora watoe maoni yao kwenye umma kwa kupitia vyombo ya habari ambapo watasikiwa na wananchi ambao kimsingi ndiyo wenye nchi.
Na hata alienda zaidi na kutukumbusha kuwa huko nyuma hata uteuzi wa viongozi kwenye taasisi nyeti ulizingatia vigezo ambavyo vilikuwa clearly stated, kama vile uzalendo (patriotism), jitihada (diligence), kutokuwa mwizi na mbinafsi.Na akaweka wazi kwa kusema hata usalama wa taifa walisaidia kuwapata viongozi wa kutimikia maeneo hayo nyeti.Lakini hivi sasa, alisema Dr Kitine, utaratibu huo haupo, mambo yanakwenda kiholela holela."Mtu yeyote atakayeonyesha kutetea maslahi ya walio wengi nchi hii siku zote ataandamwa sana, kwa hiyo inataka ujasiri sana" Mi binafsi namkubari sana Dr Kitine, na Mungu amjalie maisha marefu zaidi ili aendelee kuisaidia nchi hii kifikra.
..ukiona mtu mwenye scandals kama Kitine anapata ujasiri wa kuongea hadharani ujue hao anaowasema wamechafuka zaidi yake.
..utawala huu ungekuwa umesheheni watu wenye maadili na hekima watu kama Kitine wasingejitokeza na kuanza kuushambulia.
CCM.... bado mwingine ... Who's next Mkapa, Mwinyi, Malecela or ...
Wakati Dr. kitine anaongelewa kama shujaa, najiuliza kama ametakasika na ile shutuma ya kutumia mamilioni ya serikali kumtibu mkewe na jinsi alivyomfanyia Jenerali Ulimwengu kwa kuibua ile habari kwenye gazeti la Rai. Labda ile habari ya Kitine imeshasahaulika... Wasiwasi wangu ni kuwa isije kuwa watu wanapiga kelele kwa kuwa wako nje ya 'game' na sio kwasababu ni wazalendo.
Naye si alikuwa jasusi anajua kabisa mbinu zao, kwamba kule kwa sasa kuna kutoelewana kama ilivyo kwenye chama chao.