Wamedondosha nyingine (WAGOSI) inaitwa UPEPO SIO
Nafikiri Roma aliwapenda sana hawa jamaa na akataka afuate msimamo wao wa kuikosoa serikali. So sad serikali imemuwahi Roma. Wagosi watabaki kuwa wakosoaji pekee wa serikali wasio yumbishwa na upepo wa kisiasa
Hakika, kuna kipindi nyimbo zao zilipendwa sana japo tulizichukulia upande wa comedy jinsi walivyo act (traffic hao ngoja tijaribu kama tutapita) lakini kiuhalisia traffic ndio wanatutesa barabarani. Je, kuna funzo lolote tulilipata kutokana na wimbo huo au tulifurahia tu jinsi walivyo jazana kwenye buti? Mungu awape uhai waendelee kuwapigania wanyonge kupitia nyimbo zaoNakubaliana nawe mkuu. Wagosi ndo wasanii pekee waliobakia kuikosoa serikali kupitia sanaa. Na ni kama wapo 'makini' fulani hivi katika uwasilishaji wao wa sanaa. Huwa wapo 'non-alignment' kwenye mambo ya kisiasa, nadhani hii pia imewasaidia sana kwenye music mileage yao. Japo waliwahi kufungiwa ule wimbo wao uitwao 'Wauguzi'.
Ukisikiliza nyimbo zao kama: Lidandasi, Umeme & Maji, Waugusi, Soka la Bongo, Nyeti, n.k zinakumbusha mbali sana.
Roma yeye amekuwa 'too vocal' ... hii imechangia sana kuonekana 'anaizingua' serekali.
-Kaveli-
Washkaji zangu wawili wa maskani wanafuatilia kupata passport ili wajichanganye bondeni kwa Madiba kwenda 'kuchukua maisha'. Leo wakadondosha apdeiti maskani kuwa ni mwezi mzima sasa wanazebezwa tu na kupigwa kabobo nyepesi. Ghafula nikakumbuka 'pini' murua kabisa kutoka kwa Dr John iitwayo 'Uhamiaji', track ambayo aliipika na kui-release karibia miaka 7 iliyopita lakini hadi leo hii maudhui ya wimbo huo bado yanaakisi kabisa UHAMIAJI ya leo.
Na mara nyingi sana huwa najiuliza bila kupata majibu, WHY nyimbo 'kuntu' kama hizi huwa hazipati airtime kwenye mainstream? Ni ngoma tamu sana. Msikilize Dr John...
Ubora wa picha sio kiviile. Audio is hereby attached as well. Long live Dr. John, long live Wagosi wa Kaya a.k.a wazee wa Tanga-kunani. Huwa naenjoy sana ladha za wakongwe hawa since back in ze dei nikiwa chalii.
HIP-HOP... The good music I like most.
-Kaveli-
Tuwekee nduguWamedondosha nyingine (WAGOSI) inaitwa UPEPO SIO
Hakika, kuna kipindi nyimbo zao zilipendwa sana japo tulizichukulia upande wa comedy jinsi walivyo act (traffic hao ngoja tijaribu kama tutapita) lakini kiuhalisia traffic ndio wanatutesa barabarani. Je, kuna funzo lolote tulilipata kutokana na wimbo huo au tulifurahia tu jinsi walivyo jazana kwenye buti? Mungu awape uhai waendelee kuwapigania wanyonge kupitia nyimbo zao
Huyu jamaa ana kipaji sana inasikitisha umri unaenda na hajafaidika na ubunifu wake wa kazi..walikua wanahojiwa kwenye mkasi jamaa ni kama wamepoteza muelekeo kbs hawajui hata wafanye nini..inasikitisha!