VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,Mheshimiwa Eliezer Feleshi,amewasilisha Kusudio la kukata Rufaa dhidi ya Hukumu iliyomweka huru Prof. Costa V. Mahalu na Bi.Grace Martin. Hii inamaana kuwa Jamhuri itakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi,Ilvin Mgeta pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Kama Jamhuri,ikiwa na muda wa kutosha wa kuthibitisha shtaka pale Kisutu,ilishindwa kufanya hivyo,itaweza kuthibitisha Mahakama Kuu? DPP haoni kuwa kama hana ushahidi wa kutosheleza,Rufaa hii itagharimu fedha za walipakodi wa kitanzania bure? Kimsingi,naiona Rufaa ya DPP kama ni butu.Hatahivyo,Mahakama Kuu itatupa jibu kamili siku itakapofika...

Kesi hii haina tija kwa taifa. Ni kupoteza rasilimali za fedha na muda.
Kwanza inaonekana ipo kisiasa zaidi!
Wamewashindwa mafisadi papa na nyangumi wanadili na dagaa!
Hivi kesi ya akina Mramba imeishia wapi vile!
Mara nyingi kwa kesi kama hii ya Mahalu,serikali inaposhindwa hujidai kuwa ina appeal ruling husika lakini ukweli wa mambo ni kwamba hawafanyi hivyo na kama wakifanya hivyo inakuwa to save their face!!Ninaamini hivyo kwasababu nina mfano hai wa kesi ya aliyekuwa waziri wa miundombinu enzi za Mwinyi Nalaila Kiula; yeye alishinda kesi ya ufisadi dhidi yake na serikali ilitangaza kukata rufaa lakini toka hapo sijasikia lolote kuhusu ile kesi mpaka hivi leo na hivi sasa nasikia Kiula amempokea bwana na amekuwa mchungaji. BWANA ASIFIWE! Mahalu has no reason to worry about the appeal after all most of the people bound to hear his appeal are either his former classmates or his former students!!!!