DPP Biswalo Mganga tunaomba uwatendee haki watanzania. Viongozi wa CHADEMA waliotafuna Mali ya Umma wafikishwe Mahakamani

Taja majina mkuu chadema ni kubwa na itakua nzuri ukitaja na aina ya ubadhilifu ,na ushahidi,kamwe binafsi sipendi mtu fisadi hata siku moja
 
Kwanini unatuletea barua ya Maganga huku? Si umpelekee mwenyewe ofisini kwake?
 
DPP awafunge jera
 
Naungana na wewe lakini angeanza wale waliochota 1.5T kwa mjibu wa CAG,harafu akina Chenge na mikataba ya madini,rada,Kikwete aliyesaini mikataba ya madini inayotunyonya.Nadhani itapendeza (Shika)!!
 
Haya masuala si yalisha fikishwa takukuru na wakahojiwa sasa hiyo kazi unampa mganga ya nini wakati tayari taasisi husika ilishafanyia kazi na kama kimya maana yake ni umbeya tu kama unao utoa wewe hapa. Mtu mzima una leta umbeya? Kama una ushahidi nenda takukuru au polisi acha kuleta umbeya JF
 
Najua una hasira, ni haki yangu kutaka wahalifu washughulikiwe,usiniingilie.
 
Ni mahakama pekee ndiyo yenye haki ya kumwita mtu mhalifu baada ya kujiridhisha na ushahidi usiokuwa na mashaka wewe huna haki hiyo. Mahakama haifanyii kazi hisia au umbeya. Innocent until proven guilty!

Ndiyo maana baada ya uchunguzi Takukuru hawakuona hoja wala ushahidi wa hayo uliyo yasema. Vinginevyo kesi zingefunguliwa.

Kama una ushahidi peleka Takukuru lakini hawafanyii kazi hisia
Najua una hasira, ni haki yangu kutaka wahalifu washughulikiwe,usiniingilie.
 
Kama sio wakora, ziko wapi pesa walizochanga wabunge wa Chadema? Premafacie evidence ni kuwa hawa ni wakora.
 
Mtu akinywa supu ya utumbo ni lazima tu awe anaongea utumbo,hivi sababu yake ni nini?
 
Ulitaka ukabidhiwe wewe? Waliochanga kwa mujibu wa katiba yao hawalalamiki cha ajabu una lalamika wewe ambae hata senti moja hujachanga. Pilipili ziko shambani zina kuwashia nini?
Kama sio wakora, ziko wapi pesa walizochanga wabunge wa Chadema? Premafacie evidence ni kuwa hawa ni wakora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…