Hapa bado kwa walitajwa hapa! Binafsi namtazama zaidi Dotto Biteko na bila shaka kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu ilikuwa ni kupata uzoefu zaidi!
Ila tusubiri tuone ila kwa Makonda kazi itakuwepo, Aweso anafanya kazi nzuri ila bado kushika nyadhifa kubwa kama hii
==============
Majina ya vigogo hao watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) β
Mhe. Paul Makonda,
Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, na
Mhe. Jumaa Aweso β yameanza kutajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuteuliwa kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, endapo mabadiliko ya uongozi yatahitajika baada ya uchaguzi mkuu.
Wananchi na wachambuzi wa siasa wanasubiri kwa hamu kuona iwapo Rais Samia Suluhu Hassan atafanya mabadiliko yoyote katika safu ya juu ya uongozi wa serikali. Majina haya yameibuliwa kutokana na rekodi zao za kiuongozi, weledi na umaarufu ndani ya chama na serikali.
Paul Makonda
Aliwahi kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na baadaye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Anajulikana kwa kauli thabiti, utendaji wa haraka, na uwezo mkubwa wa kushawishi makundi ya vijana.
Dkt. Dorothy Gwajima
Ni
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Amewahi pia kushika Wizara ya Afya. Ana rekodi nzuri ya utumishi wa umma, na ni mtaalamu wa utawala wa afya kwa zaidi ya miaka 20.
Jumaa Aweso
Ni
Waziri wa Maji, anayesifika kwa usimamizi wa miradi mikubwa ya maji vijijini na mijini. Amejipatia umaarufu kutokana na ukaribu wake na wananchi na uwezo wa kusimamia utekelezaji wa sera
Je ni yupi anafaa endapo ikitokea kama inavyosemekana* ?
View attachment 3497300View attachment 3497301View attachment 3497302?