You have spoken it all Dr. W. P. Slaa. Simba,Yanga na jamaa fulani hivi ndiyo laana ya nchi hii.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa, amezitolea uvivu klabu za Simba na Yanga kusema hazina jipya.
Slaa alitoa kauli hiyo juzi Jumapili kwenye mkutano wa kumpongeza mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kibwegere, Edson Nyingi, uliofanyika kwenye viwanja vya Makombe, Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo, Dk. Slaa alisema kwa sababu Simba na Yanga zimeshindwa kufika popote, ni lazima zitafutwe timu mbadala za kuweza kuchukua nafasi zao.
Alisema anasikitishwa na klabu hizo kwani licha ya ukongwe zilionao katika Soka la Tanzania zimeshindwa kuitangaza nchi kimataifa.
"Sina ugomvi na Simba wala Yanga, lakini lazima tukubaliane kuwa zimeshindwa kuitangaza nchi kimataifa na hii ni kutokana na mipango mibovu ya klabu hizi, hivyo ni wakati wa vijana kujipanga kuanzisha timu zenye malengo.
"Angalia Azam, licha ya kwamba ni timu changa iliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni, lakini imeonyesha dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo ya soka kama tunavyoshuhudia tayari wana uwanja wao," alisema Dk. Slaa.
"Wana vitendea kazi vingi na wapo wanazingatia soka la vijana lakini Simba na Yanga ziko pale pale miaka nenda rudi, ni dhahiri kwa mwenendo huu hawatafika."
Chanzo: Mtanzania
mbona chadema kinamika ishirini hata hiyo tv na jengo la makao makuu hawana.
mzee slaa wa ajabu sana anajadili mpira wakati hakucheza hata mpira wa matambala hakucheza.
Mpwa naskia hii katuni ndio iliyoacha Mwambene "alimbene" lile gazeti la kizungu ujue, shauri yako
Naamin wamemquote vibaya...kwa mwanasiasa mkubwa kama Dr Slaa ni risk kubwa kuziponda timu zenye wapiga kura wengi.
Masuke Tanzania Michezo ni siasaWanasiasa bana watu wa ajabu sana, wanajifanya kila kitu wanajua. Imarisheni ya kwenu kwenye siasa, mmeshatuvuruga kwenye siasa mmetosha, msitake kutuvuruga na huku. Nyie mnapewa ruzuku ya kodi zetu lakini hakuna lolote mnafanya itabidi na sisi tuanze kuidai serikali angalau ianze kutoa ruzuku kwenye timu za ligi kuu.
Ni rahisi kutokea kwenye mpira kwenda kwenye siasa na sio kinyume chake.Masuke Tanzania Michezo ni siasa
- Gulamali alienda Yanga akagombea Ifakara
- Shabib alifadhili simba sasa ni Mbunge Gairo
- Rage...........................
- Manji alijaribu Kigamboni
- Mwakalebela.............Iringa
- ..............sasa Malinzi anaenda Bukoba mjini na hata Kagasheki anajua
- you name the,...............................
ndio maan hata mpira ni siasa