...............duuuuuh!! kazi tunayo watanzania, nilikuwa sijui kuwa ignorance rate ni kubwa kiasi hiki hadi kwenye mitandano ambayo tunadhania wapo ''Great Thinkers'' halafu tunashuhudia umbu mbu mbu wa aina hii lol!!. Tuzidi kumuomba Mungu atupunguzie hii adhabu ya kutotumia ubongo kufikiria na atuchagulie adhabu nyingine yoyote ile hata kilema au kifo. Yaani unamfananisha Lema na Ponda au Fareed? Ok, Lema ni kiongozi wa Chama Cha Chadema ambacho ni cha kisiasa, je Punda na Fareed ni viongozi wa vyama gani vya siasa? Au mnataka kuvuta hisia za watu kwa kujaribu kuunganisha matukio ya kisiasa na kidini? Kweli wakati watu wengine wakiomba heri wanyimwe mali wapewe akili, kuna wengine wanaomba heri wanyimwe akili lakini wapewe Midevu lol!!Kwani ww ulie andika hapa mbona nimtu ambaye hujui unaloliandika hapa Arusha kunasiku watu wamevamia eneo la kilombero wakavunja wakaiba mabati wakajipimia maeneo yao na mshawishi wa mambo hayo ni LEMA watu kimya lakini SHEIKH PONDA kavamia na mchochezi LEMA yeye mtusafi anapeta tu lakini iko siku haki itapatikana
habari za jumapili.
Tafadhali mno naomba kujuzwa kwa kifupi mno vurugu zilizotokea mwebechai miaka ya tisini, katika maeneo yafuatayo;
1. Nini kilikuwa chanzo cha vurugu hizo.
2. Athari zake hasahasa vifo, ulemavu wa kudumu.
3. Wahusika walichukuliwa hatua gani?
4. Kuna uhusiano kati ya tukio hili na lile la kuvunja mabucha ya nyama ya nguruwe? au ni moja tu.
5. Na kingine chochote lakini hususani hayo hapo juu.
Nilikuwa mtoto kipindi hicho kuweza kujua na pia nimefatilia katika mitandao ikiwemo jf lakini sikushiba vizuri. Najua humu kuna watu walikuwepo wanaweza kata kiu yangu.
Ahsanten.
Amin,Amina
BACK TANGANYIKA
Nimekua kila siku upande fulani kwa kila likitokea jambo
Lakini sasa naona hatari ya kuendelea na msimamo huu
kwani walipouliwa waislam mwembechai, wapo walioumia na wapo walioguswa na kusikitika kuona hawakutendewa haki kwani mambo waliyoambiwa ni uzushi
ikafuata wapemba baada ya uchaguzi waliuliwa kama mbuzi na kukimbilia mombasa ikawa sawa kuwa hao niwana CUF wamejitakia wneyewe
Kubenea naye kutetea haki hakuachwa wengi tulimuona amejitakia kwani hatuhusu
ikaja chadema arusha hapo tukaanza kupata picha kumbe hili SERIKALI katili halina huruma na linavunja haki za binadamu, kufumba na kufumbua morogoro na ikamaliza na iringa sasa chadema kimya
ulimboka na wenzake wakidai maslah yao ya msongi naye yakamkuta tuasema amejitakia kwani anasumbua nchi na kuhatarisha amani ya nchi
sasa ponda na farid twasema sawa hawa kwanza magaidi ni stahili yao wauwawe na kuwekwa ndani forever
hii hali ni mbaya kwani serikali inatumia loop hole hii ya kundi moja kua inaunga mkono serikaili inaposhughulia kundi jingine.
watanzania tunatakiwa kuacha kua bias tuyaangalie mambo kwa jicho la haki hasa inapokuja suala la uhai wa mtanzania, ni kweli hao wote walikosea kudai mambo kadhaa kwa serikali iyarekebishe? serikali hii kwa mitndo huu tujue itatumaliza ikimaliza kwa hao wewe na mimi tujue siku moja nasi yatatufika, tupendane na tuone umuhimu wa mtu kutundewa haki na tusiwe mashabiki
Hii ni ushauri si lazima uukubali leo hata baadae ukiwa peke yako utaona ipo shida kwenye uongozi wetu na tukicheka nao tutaambulia patupu