Kwamba ipo siku utakufa.
Sote tutakufa.
_____
Amani iwe kwenu.
Huu ndiyo ukweli usiopingika, uwe mwenye imani kuwa Mwenyezi Mungu yupo au la, siku itafika utakufa.
Ule vizuri, ufanye mazoezi, ufanye yote utakayoweza hapa duniani lakini ipo siku utakufa.
Kifo ni mawaidha mujarabu kwa wenye imani na uwepo wa Mwenyezi Mungu.
Tujitahidi kuacha kufanya mabaya na tujitahidi kutenda yaliyo mema na kufanya ibada mbalimbali.
Katika mitihani ya masomoni huwa tunapewa maswali na muda lakini tunafichwa majibu, ila katika maisha ya imani za kidini 'tumepewa maswali na majibu', lakini tumenyimwa muda!
Tuwaidhike (lets take heed)
Hatujui siku wala saa.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwa hakika kwake tutarejea.
decomm!