Baba wa Taifa letu (RIP) ulituachia madini ili baadae tuje tuyatumia sasa hivi wanatumia wenye macho, ulisisitiza watoto wa taifa hili wasome na uliwapatia kazi walipomaliza masomo, sasa hivi wako mitaani hawana kazi, uliacha mtu akifika miaka hamsini anastaafu kwa hiari, hamsini na tano kwa lazima siku hizi si hivyo tena ni sitini akifa ndio tunaambiwa ukweli kwamba alikuwa na sitini na nane. watoto wao wamejaa maofisini wetu wanasubiri wajanja waanzishe maandamano na wao washiriki, yale mashirika uliyosema yasibinafsishwe ulipokufa tu yakabinafsishwa yote. mfano Tanganyika Packers imekuwa gofu na hii imesababisha ugomvi wa wafugaji na wakulima maana wakati ule ng'ombe ziliuzwa huko, sasa hakuna pakuzipeleka, Uliacha TIPER sasa hivi ni sehemu ya kuhifadhi mafuta ya wajanja, kiwanda cha lami kimekufa kikiwa bado kipya kabisa na hakuna anayekiongelea tena. Uliahidi utatuombea, tuombee huu mzimu wa UMIMI utoweka katika taifa hili.