Dear Atheists, this thread’s for you — Everyone else, keep scrolling!

Mkuu hebu fikiria ikiwa hapo huwezi kumfanya Rais Samia kuja kujieleza kwako kwa lolote kwanini unadhani Mungu ndio analazimika kuja kujieleza kwako?
Raisi Samia yupo.

Mungu hayupo.
 
Kwanini mnapenda sana kumtetea mungu?
ina maana yeye hawezi kujitetea mpaka Aweke wawakilishi machawa kama nyie ndo tumjue!?

Haya nikuulize ulishawahi kumuona shetani au malaika?
Ukiachana na huyo mungu wako?
 
Your God is useless..🚮
 
Umesema Rais Samia yupo, ndio nimekuuliza je unaweza kumfanya aje akujibu hoja yeyote kama kweli yupo?
Unacho taka wewe ni kuunda mifano ambayo ni illogical kuihusisha na kufananisha na concept ya huyo Mungu.

Rais Samia yupo na anathibitishika yupo.

Mungu hayupo na wala huwezi kuthibitisha yupo.

Usitafute mifano uchwara isiyo na mantiki.
 
Unacho taka wewe ni kuunda mifano ambayo ni illogical kuihusisha na kufananisha na concept ya huyo Mungu.

Rais Samia yupo na anathibitishika yupo.

Mungu hayupo na wala huwezi kuthibitisha yupo.

Usitafute mifano uchwara isiyo na mantiki.
Wewe unataka hadi Mungu aje kwako kujieleza ndio ukubali kuwa yupo, nikakwambia hoja yako hiyo haina mashiko kwa sababu haiwezekani et Mungu aje kujieleza mbele yako kwani wewe nani? Na ndio maana nikakupa mfano wa Rais Samia kuwa pamoja na kuwa unasema yupo ila huwezi kumtaka aje kwako kujieleza kwa lolote, sasa iweje wewe ujenge hoja ya kwamba et ili ithibitike Mungu yupo basi et aje kwako kujieleza mwenyewe.

Sijui kama umeelewa?
 
Mungu hayupo ni nyie tu mnahangaika kumwelezea na kumtetea kufosi aonekane yupo.
 
Mungu hayupo ni nyie tu mnahangaika kumwelezea na kumtetea kufosi aonekane yupo.
Mimi nadhani wewe ndio unajihangaisha kutaka kulazimisha watu wakubali unachoona wewe kuwa ndio kiwe ukweli. Kama wewe unaona madai ya kwamba hakuna Mungu ni ya uhakika pasina shaka basi hadi sasa kusingekuwa na watu wenye kusema Mungu yupo kama ambavyo hadi sasa hakuna tena anayesema 2pac bado yupo au Osama bin Laden yupo.
 
Wapi nimekulazimisha?

Ninyi ndio kila siku mnahangaika kuanzisha nyuzi za kuwaita Atheists.

Hata huu uzi umeanzishwa kwa sababu ya Atheists.

Ninyi ndio mnalazimisha, mnahangaika na mnafosi uwepo wa huyo Mungu.

Uthibitisho wa Tupac upo hata picha zake zipo, nyimbo zake zipo, albamu zake zipo. Huu ni uthibitisho tosha kwamba Tupac alikuwepo.

Picha za Osama zipo, documentary zake zipo na zinatoa uthibitisho tosha kwamba Osama alikuwepo.

Hakuna uthibitisho wowote ule wa uwepo wa huyo Mungu.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Your God is useless..🚮
My friend, you can call God “useless,” but I’ve seen Him heal, restore, provide, and transform lives — including mine. That’s more than any insult or emoji can erase.

Mockery doesn’t change reality. You dismiss what you don’t understand, but that doesn’t make it meaningless — it just shows you haven’t experienced it yet.

You may mock now, but when life brings you to a place your logic and pride can’t fix — remember, the same God you called "useless" will still be merciful enough to hear you if you call on Him.
 
Una tatizo la kushindwa kuelewa unachosoma, nimekwambia hivi wewe umejipa uhakika kabisa kuwa huyo Mungu hayupo na si vinginevyo na ndio nikasema kama Mungu hayupo na huo ni uhakika bila ya shaka basi hadi sasa kusingekuwepo na watu wenye kuendelea kudai Mungu yupo. Nimetoa mfano wa 2pac ambaye alipokufa kuna watu walikuwa wanadai hakufa yupo hai ila hakuwahi kuonekana tena 2pac hadi leo na hivyo hakuna tena madai ya kwamba 2pac hakufa na kwamba yupo hai.

Sasa wewe kwa kushindwa kuelewa kwako unakuja kusema sijui picha za 2pac zipo mara album zake zipo kuthibitisha alikuwepo, wakati mimi nazungumzia madai ya watu waliyokuwa wakisema hakufa bado yupo.

Halafu kwani huyo babu mzaa babu zako unazo picha zake za kuthibitisha alikuwepo?
 
Kudai, unaweza hata kudai uwepo wa kitu au jambo la uongo lisikuwepo.

Hata mimi naweza nikadai kuna Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao.

Lakini kiuhalisia hakuna Dragons watemao moto midomoni mwao.

Ni stori na hadithi za vitabuni tu.

Hivyo hivyo kwa huyo Mungu wenu mnayedai yupo kila siku. Hayupo katika uhalisia bali ni stori na hadithi za vitabuni tu.

Kwa hiyo watu wengi kudai Mungu yupo, Hakufanyi Mungu huyo awepo kweli. Mungu huyo ni hadithi za vitabuni tu.

Hakuna Mungu.
 
Mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu,jamani tusikibali kuwa wapumbavu.
 
Wewe umejuaje hakuna kweli huyo Mungu? Maana kusema tu kitu hakipo hakifanyi kutokuwepo hicho kitu na ndio maana kuna watu walizushiwa kifo ila baadaye wakaonekana wakiwa hai.

Hauna huo uhakika wa kwamba huyo Mungu hayupo kweli hivyo huko kusema hakuna Mungu ni aina ya mtazamo tu ambao umeukuta na kuchagua kuufuata ni sawa tu na wale waliyofuata mtazamo wa kwamba Mungu hana dini.
 
Wewe umejuaje hakuna kweli huyo Mungu?
Utajuaje kisichokuwepo?

Utatumia namna gani kujua kisicho kuwepo?
Maana kusema tu kitu hakipo hakifanyi kutokuwepo hicho kitu na ndio maana kuna watu walizushiwa kifo ila baadaye wakaonekana wakiwa hai.
Hapa tunazungumzia Mungu.

Usilete mifano illogical kuihusisha na Mungu.
Hauna huo uhakika wa kwamba huyo Mungu hayupo kweli hivyo huko kusema hakuna Mungu ni aina ya mtazamo tu ambao umeukuta na kuchagua kuufuata ni sawa tu na wale waliyofuata mtazamo wa kwamba Mungu hana dini.
Mungu hayupo nina uhakika.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Ukibisha thibitisha Mungu yupo.

Na ueleze huyo Mungu yupo kwa namna gani?

Usilete mifano ambayo haina mantiki kuanza kutetea uwepo wa huyo Mungu.

Mthibitishe huyo Mungu yeye kama yeye.
 
Sawa mie sileti mifano si unakataa mifano, haya niambie huo uhakika wako wa kuwa Mungu hayupo umeupata vp? Kwa sababu wewe umezaliwa umekuta teyari kuna wenye kudai kuna Mungu na kuna wenye kudai hakuna Mungu, sasa wewe ulipata vp uhakika wa kwamba hakuna Mungu?

Haya eleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…