DC Makonda abanwa Kortini leo

Ikiwa ni siku ya makonda kujitetea nani anapaswa kujitetea mahakamani mlalamikaji au mtuhumiwa maana naona umetuletea pumba tu hapa.ungepaswa kusema Leo ilikuwa ni siku ya ushahidi ambapo mlalamikaji ametoa ushahidi wake mahkamani kuhusu kesi Flani.
usishangae mkuu kibao kimegeuka ! kuna kila dalili ya makonda kudhalilika zaidi .
 
Ikiwa ni siku ya makonda kujitetea nani anapaswa kujitetea mahakamani mlalamikaji au mtuhumiwa maana naona umetuletea pumba tu hapa.ungepaswa kusema Leo ilikuwa ni siku ya ushahidi ambapo mlalamikaji ametoa ushahidi wake mahkamani kuhusu kesi Flani.
Soma vyema hoja kabla hujatoa maoni, na pia jifunze taratibu za mahakama. Mfano mlalamikaji au shahidi huulizwa maswali na upande wa pili.
 
Hilo linafahamika ila unapaswa kujua mshtakiwa haulizwi swali na mlalamikaji wakati wake wa utetezi ukifika ila mleta hoja anasema NI SIKU YA MAKONDA KUJITETEA na sio kwamba ni siku ya kutoa ushahidi KUJITETEA ni kitendo kinachofanywa na mshtakiwa na huwa hadi kufikia hatua hii mahakama imeshafunga ushahidi wa kesi flani.lkn pia mlalamikaji huwa hajitetei bali anatoa ushahidi wkt mshtakiwa ndio anajitetea baada ya ushahidi kumalizika kusikilizwa sasa hoja yangu ni kuwa makonda kwa kesi hii sio anayejitetea bali yeye anatoa ushahidi tu.
 
hakimu anaapoteza mda kusikiliza kesi ya konda isiyo na mbele wala nyuma
 
Leo mahakamani aise.Makonda jasho lilimtoka

Mwanasheria..brother Makonda,unafahamu vigezo vya uteuzi mtu awe mkuu wa wilaya?

Dc Makonda....Sijui.

Mwanasheria. Je unafahamu nini maana ya mjinga?

Dc makonda Kimya...

Mwanasheria....je unaweza ukakubaliana na mimi...kuwa ili mtu awe mjinga...inategemea kwa jambo flani...kutokulijua. .je....wewe kwa kuambiwa. MJINGA..kwa sababj hufahamu uteuzi wako umeteuliwaje kuna tatizo?

Dc makonda = kimyaaaa

Je wewe ndiye ulitoa amri kubenea akamatwe?
Dc makonda...sio mimi....


Mwanasheria ....nani aliyetoa amri kubenea akamatwe....


Dc makonda....akajibu...ni afisa upelelezi wa Magomeni ndiye aliyemkamata Kubenea....

....Ha ha ha ha....

Patamu.....

Simalizi uondo...nisije nikaingilie uhuru wa mahakamani bure.

KESHO SAA MBILI ASUBUI.....

MAHAKAMA YA KISUTU...


BY PERFECT.MWASIWELWA.

ADMIN MAKINI
 
Samahani wanabodi hii kesi ni ya Madai au Jinai?
 
Mbona Mkapa alivyowaita wajinga mlikuwa wakali mpaka Mbowe akatoa tamko.

Kwa kifupi hii kesi ngumu sana kwa Kubenea.
mimi ni mwanasheria, nazungumzia upande huo. hata witness aliyempeleka ambaye ni dc sio credible. evidence atakazotoa ni admissible but not liable.
 
mtoa mada hujui maswali ya mahakamani mimi naona dc makonda muelewa kuliko kibatali kwa maana swali lisilo la msingi hakujibu
 
Mleta mada kaleta uzi huku tayari akiwa na upande anaoushabikia...hivyo kufunga uhuru wa wadau kutoa maoni yao hata kama walikuwapo mahakamani......hili suala lipo kitaaluma zaidi halipo kishabiki ingefaa wadau wenye taaluma ya sheria na kama walikuwapo mahakamani watupe muendelezo wa kesi inavyoenda na kwa usawa na kwa haki.....

Kwa namna yoyote ile matumizi ya lugha chafu si sehemu ya maisha ya waungwana hasa kwa mtu mwenye hadhi ya ubunge kama alivyo mbunge wangu kubenea......

Busara zaidi ingetumika badala ya jazba isingefikia huku.....

Huo muda mnaoupoteza mahakamani ni muda ambao mngepaswa kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo......kufanya hivyo ni kuwadhurumu wananchi muda wao wa kuwatumikia kama muwakilishi wao hivyo kuchelewesha mipango ya kimaendeleo uliyojiwekea kwa wapiga kura wako.....

Kila mmoja amemkosea mwenzake kwa namna moja au nyingine lakini matumizi ya jazba na ubabe ndio vinewafikisha hapo....wote wakiwa viongozi wanaowarumikia wananchi kwa namna moja au nyingine wangepaswa kulimaliza kiutu uzima ikizingatiwa kuwa kupishana kauli ni jambo la kawaida kwa wanaadamu wasio wakamilifu.......
Vile vile vijana wajifunze kutumia bongo zao vyema na sio kupelekwa pelekwa na upepo wa kisiasa kama bendera hata kushabikia mambo ya kipuuzi eti kwa kuwa ni mtu aliyepo upande wako wa kisiasa.....kwenye nyeusi isemwe ni nyeusi kwa kuwa inaonekana hata kwa macho kuwa ni nyeusi...nasisitiza tena matumizi ya lugha chafu dhidi ya mwenzio ni jambo baya na si la kiungwana....nina hakika hata wewe unayemshabikia Kubenea kwa kutoa lugha hiyo dhidi ya makonda( kama kweli aliitoa maana sikuwepo eneo la tukio) usingefurahia na ungeonesha kuchukuzwa na hilo........

MATUMIZI SAHIHI YA UBONGO WETU HUTUFANYA KUWA NA HEKIMA NA BUSARA....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…