Dawa ya Kwikwi ya Muda Mrefu

Dawa ya Kwikwi ya Muda Mrefu

Tujikomboe Finance

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
212
Reaction score
81
Naomba kusaidiwa dawa ya kwikwi ambayo imedumu muda mrefu zaidi ya miaka mitano

Iwe ni dawa ya hospital au tiba mbadala
 
mmmh pole sana..nenda hospital kachunguze, kwikwi ya miaka mitano hiyo siyo ya kawaida
 
Kuna ndugu yangu ana tatizo ilo...ata anywe maji wapi ukimstua wapi ipo....anapatwa na kwikwi ata masaa4 ndio inatulia
 
Ukipata tukio lolote ukalia kwikwi itaisha hapo hapo.Njia ingine ingiza mkono kwenye kwapa lako hasa wakati wa jua kali koroga mkono wako kwapani uzoe harufu yote kisha nusa utaniambia habari yake . ila tiba hizi ni kwikwi fupi fupi miaka mi5 noma
 
Naomba kusaidiwa dawa ya kwikwi ambayo imedumu muda mrefu zaidi ya miaka mitano

Iwe ni dawa ya hospital au tiba mbadala
Mimi nilipata kwikwi ya wiki mbili nilienda hosp walinipa vidonge 2 vidonda wakasema nimeze vyote nikameza pale pale,, kilichonipata sikufika hom mwili wote uliisha nguvu, kizunguzungu nilipofika hom, nililala siku 2, sikuweza kwenda hata dukan,
Baada ya hapo kwikwi ilipona mpka leo siijui
 
Fanya hivi:Chukua maji ya kunywa ktk glasi.Kunywa yote taaaaratibu sana bila kutoa pumzi au kuingiza pumzi mpaka yaishe.Inasaidia.
Nimejaribu mbinu zote za asili lkn imeshindikana. Ngoja nijaribu hii ya kunywa maji. Siku ya pili leo nateseka na kwikwi.
 
Saa hizi saa sita na dakika 14,kwikwi inanitesa balaa,sijui ntafikaje asubuhi.
 
Saa hizi saa sita na dakika 14,kwikwi inanitesa balaa,sijui ntafikaje asubuhi.
Pole,
Kuna sababu za muda mfupi na muda mrefu zinazosababisha kwikwi. Kuna sababu zinazoweza kuondoka zenyewe na kuna zinazohitaji kufanyiwa tiba ili kuondoa kwikwi na sababu yake.

A: Kwikwi ya muda mfupi/chini ya saa 6, unaweza kutumia njia za asili kama:
1: kunywa maji
2: kuacha kupumua kwa muda/ kushikilia pumzi kwa muda.
3: kuweka maji kwenye beseni na kuweka uso wako.
4: kufanya kama unasukutua maji kwenye koo/giggling nk.

Njia ya asili inaposhindikana ni vyema kufika kituo cha afya ambapo utapata kuangaliwa vyema na kupewa tiba halisi na ikiwezekana kupewa tiba ya chanzo cha kwikwi.

B: Kwa kwikwi ya muda mrefu/zaidi ya saa sita au inayokufanya ushindwe kula/kupumua/kulala au iliyoshindikana kuondoka kwa tiba ya asili:
Ni vyema kufika hospitali na kuangaliwa ni nini chaweza kuwa ni sababu. Ni muhimu ili pamoja na tiba ya msingi, pia utahitaji kufanyiwa tiba ya chanzo cha kwikwi. Kwikwi ya muda mrefu yaweza kuwa ni ishara ya tatizo jingine muhimu kutatuliwa kama:
1: shida ya figo
2: shida ya sikio
3: shida ya njia ya chakula
4: shida ya ubongo
5: shida ya madini mwilini nk.

Kuna dawa za aina mbalimbali ambazo huweza kuzuia au kuondoa kwikwi. Dawa hizi zimekuwa zikitumika pia kwa kazi nyingine kama:
1: kulainisha misuli
2: kuzuia kutapika

NB: Dawa na utaratibu wa kuondoa kwikwi upo, ila suala kuu ni kuzingatia mwenendo mzima wa kwikwi na hali ya mgonjwa husika.
 
Asante sana kwa maelezo na ufafanuzi uliotoa,kwikwi ilinianza saa tisa jioni,ikaendelea hadi kumi na moja jioni,baadae ndiyo ikaja kujirudia tena saa nne usiku ikakata saa saba usiku.
Kwa maelezo uliyoyatoa,itabidi niende kesho hospitali,nilaonane na tabibu.Asante sana.
Pole,
Kuna sababu za muda mfupi na muda mrefu zinazosababisha kwikwi. Kuna sababu zinazoweza kuondoka zenyewe na kuna zinazohitaji kufanyiwa tiba ili kuondoa kwikwi na sababu yake.

A: Kwikwi ya muda mfupi/chini ya saa 6, unaweza kutumia njia za asili kama:
1: kunywa maji
2: kuacha kupumua kwa muda/ kushikilia pumzi kwa muda.
3: kuweka maji kwenye beseni na kuweka uso wako.
4: kufanya kama unasukutua maji kwenye koo/giggling nk.

Njia ya asili inaposhindikana ni vyema kufika kituo cha afya ambapo utapata kuangaliwa vyema na kupewa tiba halisi na ikiwezekana kupewa tiba ya chanzo cha kwikwi.

B: Kwa kwikwi ya muda mrefu/zaidi ya saa sita au iliyoshindikana kuondoka kwa tiba ya asili:
Ni vyema kufika hospitali na kuangaliwa ni nini chaweza kuwa ni sababu. Ni muhimu ili pamoja na tiba ya msingi, pia utahitaji kufanyiwa tiba ya chanzo cha kwikwi. Kwikwi ya muda mrefu yaweza kuwa ni ishara ya tatizo jingine muhimu kutatuliwa kama:
1: shida ya figo
2: shida ya sikio
3: shida ya njia ya chakula
4: shida ya ubongo
5: shida ya madini mwilini nk.

Kuna dawa za aina mbalimbali ambazo huweza kuzuia au kuondoa kwikwi. Dawa hizi zimekuwa zikitumika pia kwa kazi nyingine kama:
1: kulainisha misuli
2: kuzuia kutapika

NB: Dawa na utaratibu wa kuondoa kwikwi upo, ila suala kuu ni kuzingatia mwenendo mzima wa kwikwi na hali ya mgonjwa husika.
 
Jaribu kutumia jani la mgomba kunywea maji mara kwa mara sababu ni la muda mrefu pia pendelea kunywa maji ya kilimanjaro zikidndda hzo nitafute zaid

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom