Dawa ya kuzuia kutapika kwa mjamzito

saratoga1285

Member
Dec 15, 2016
29
18
Msaada mke wangu ni mjamziyo wa miezi miwili,anatapika sana npo nae hospitali toka juzi,anatapika sana chochote atakachokipitisha mdomoni lazima kirudi. Kuna MTU kaniambia nimchemshie tangawizi ya moto anywe itamsaidia kupunguza kutapika.
 
poleni. ndiyo ginger tea/ chai ya tangawizi husaidia wengi katika hicho kipindi.. ila kama anatapika kila kitu na sana basi ni vyema apewe dawa za mishipa kwanza kupunguza rate ya kutapika.. eg Ondasetron 8mg iv halafu vidonge vyake baadaye ama vidonge vya Nosic.. kikukbwa ni kuhakikisha maji na madini anayopoteza akitapika yanakuwa replaced mwilini la sivyo atanyong'onyea na kuzidiwa zaidi
 
Na azingatie sana kiumbe aliyepo tumboni, kila dawa atakayopewa a google kujua side effect ya kababy! Tumpe hongera nyingi sana na Mola awalinde mama na mtoto!
 
Usiogope hiyo hali itaisha tu, epuka dawa dawa za hospitali zitamharibu mtoto aliye tumboni hata vile vidonge vya Nosic vinazuia kutapika lakini vina madhara sana bora asitumie hiyo itaisha yenyewe mwili ukizoea, ale tu juices za malimao, ukwaju nk na usiweke sukari.
 
Mimi hutumia Nosc kuanzia miezi mi 3 ya mimba mpaka kujifungua maana huwa natapika kila nilacho mpaka naishiwaga nguvu hebu nitonye hayo madhara
 
Msaada mke wangu ni mjamziyo wa miezi miwili,anatapika sana npo nae hospitali toka juzi,anatapika sana chochote atakachokipitisha mdomoni lazima kirudi. Kuna MTU kaniambia nimchemshie tangawizi ya moto anywe itamsaidia kupunguza kutapika.
Apate glucose pamoja na ORS ya kutosha,upungufu Wa sukari na madini mwilini huwa ndo chanzo cha tatizo,pia dawa ya "vomidoxin " ni nzuri tu,ina mchanganyiko Wa vitamin B6 pamoja na Meclizine.Dawa naomba ufanye kuwa chaguo la mwisho kabisa,cha msingi ni hizo Ors na Glucose.
 
Mimi hutumia Nosc kuanzia miezi mi 3 ya mimba mpaka kujifungua maana huwa natapika kila nilacho mpaka naishiwaga nguvu hebu nitonye hayo madhara
Nosic inakuwa na vitamin b6 pamoja na dawa nyingine ya kuzuia mzio"antihistamine/anti allergy "doxylamine.That's all.
 
First trimister (14weeks) zikiisha atakuwa vizuri. Pia wanashauri usimpatie vitu vichachu maaana havita msaidia sana. Anywe maji mengi glucose kwa sana, machungwa, ikiwezekana mpatie Pregnant care maana anaweza kuwa amepoteza/hajapata madini na vit kutokana na kutapika. kumbuka mtoto anatengenezwa first trimister huko kwengine ni ukuaji tu. Hivyo ni kipindi muhimu sana kupata balanced diet.
 
Msaada mke wangu ni mjamziyo wa miezi miwili,anatapika sana npo nae hospitali toka juzi,anatapika sana chochote atakachokipitisha mdomoni lazima kirudi. Kuna MTU kaniambia nimchemshie tangawizi ya moto anywe itamsaidia kupunguza kutapika.
Pole sana, Kwa kitaalamu tunaita hyperemesis gravidarum, yaani mama mjamzito anatapika kupita kiasi ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito na baadae hutoweka , na huambatana na udhia mwingine.
Sababu kubwa ni (hCG). Hii ni hormone ambayo huzalishwa wakati wa ujauzito toka kwenye placenta. Ikizalishwa kwa wingi huweza kusababishwa hilo tatizo la kutapika sana! Hasa kwa mtu mwenye mimba ya kwanza, mwenye mapacha na mama ambae yuko overweight (obesity)
Hyperemesis gravidarum haina tiba maalumu, bali unatibu complications, kama dehydration unatoa fluids, vitamins and minerals suprementary pia kama kuna upungufu wake!
Hayo tuu!
 
Back
Top Bottom