DARUSO ni Chama Gani?

mwankuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2010
Posts
334
Reaction score
120
DARUSO NI CHAMA GANI?

Mwaka 1966 unabaki kwenye kumbukumbu katika vitabu vyetu vya historia.Mapema mwaka 1966 wanafunzi wa UDSM walifanya mgomo mkubwa ambao ulitikisa Taifa.Mgomo huu unabaki kuwa wa pekee katika historia ya UDSM na Taifa kwa ujumla,kwa sababu kuu mbili.Madai ya mgomo wenyewe na matokeo yake.

Madai ya mgomo huo,pamoja na mambo mengine,ilikuwa ni pengo la walionacho na wasionacho kuongezeka,wanafunzi kujiunga na National Service wanapomaliza masomo na kulipwa asilimia 40 ya mshahara huku viongozi wengine wakiogelea kwenye utajili.

Inasemekana Mwalimu Nyerere alichukuzwa sana na mgomo huo,hasa baadhi ya mabango ,moja likiwa na ujumbe “BORA ENZI ZA UKOLONI”.Baadaye chuo kilifungwa karibia mwaka mmoja,na Mwalimu Nyerere alipunguza mshahara wake kwa asimilia 20.
Mwaka mmoja baadaye (1967) likazaliwa Azimio la Arusha likiwa na majibu ya baadhi ya hoja za wanafunzi.Kwa mantiki hiyo,mgomo wa UDSM ulipelekea kuzaliwa kwa Azimio la Arusha kwa kiasi fulani.

Mwaka 978,wanafunzi wa UDSM wakawa mtaani tena.Dhima ya mgomo huo ilikuwa kupinga wabunge kujiongezea mishahara huku wananchi wakiishi maisha duni.Inasemekana mgomo huu uliungwa mkono sana na wananchi.Hiyo ni mifano tu ya mtiririko wa migomo katika chuo cha umma (UDSM).

Katika migomo yote hii,DARUSO ndio waratibu na waendesha migomo.Pamoja na kwamba migomo mingi hufanyika kwa pressure ya wanafunzi,mgomo hauwezi kufanikiwa bila DARUSO imara na baraka zake.

Mgomo wowote ni batili,kama bunge la wanafunzi halijapitisha.Kwa maana hiyo chama cha wanafunzi lazima kiwe imara.Kwa sasa migomo mingi inayotokea UDSM na vyuo vingine ni kwa sababu mbili.Ubovu wa Menejimenti ya vyuo na vyama vya wanafunzi.
Leo hii imekuwa rahisi sana kutabiri mgomo utatokea lini.

Wakati migomo ya zamani ilikuwa kwa masilahi mapana ya Taifa,migomo ya sasa inatokana na wanafunzi kuwa wabinafsi kwa kujifikiria wenyewe.Migomo ya sasa ni kwa ajili ya boom,na si vinginevyo.Ndio maana nasema migomo ya sasa inatabirika.Kama wanafunzi hawajapata boom basi tegemea mgomo au wanapokaribia mitihani.

Haya yanasababishwa na aina ya wanafunzi tulionao kwa sasa na vyama vya wanafunzi kama DARUSO.Wakati ule tukiwa wadogo,ukimwona kiongozi wa DARUSO kwenye TV au hata kusoma kwenye magazeti ulikuwa unatamani muda uende haraka ili nawe ujiunge na UDSM.

Jinsi walivyokuwa wanatoa hoja kwa mpangilio na kuzitetea ungetamani tu.Mwanafuzi akiwa waziri katika serikali ya DARUSO,ingesema pengine anafaa kuwa waziri katika serikali siku zijazo.Lakini haya yote yamepotea.Viongozi wa vyama hivi,hautamani hata kuwasikiliza,sembuse kuwaona.

DARUSO na vyama vingine vya wanafunzi ni kama vyama vya siasa.Leo huwezi kupata uongozi katika vyama hivi ni kazi ngumu ambayo inaambatana na matumizi makubwa ya pesa.Ninachojiuliza,wanafunzi hawa wanapata wapi fedha hizo?

Lakini pia,nyuma ya vyama vya wanafunzi kuna vyama vya siasa hasa CCM na CHADEMA.CCM na CHADEMA kwa kujua ama kutojua wameamua kuvuruga elimu yetu kwa kuwatumia vijana wa vyuo kwenye siasa badala ya taaluma.

Waafunzi wengi wamejikuta wakijihusisha zaidi kwenye siasa kuliko hata masomo.Hata maswala madogo ambayo yangeweza hata kumalizwa kwa mazungumzo yanashindikana na kupelekea migomo isiyokuwa na ulazima.

Viongozi wengi wa vyama vya wanafunzi wanatumikia vyama vya siasa.Na sasa imekuwa kawaida tu na kujitambulisha kwa itikadi ya vyama.Ni wawakilishi wa vyama vya siasa kuliko wanafunzi waliowachagua.Wengi wao wanaahidiwa vyeo,baaada ya kumaliza masomo.

Wakimaliza masomo,wengi wa viongozi wa vyama vya wanafunzi hujiunga na vyama vya siasa,na hata wanapokuwa wanafunzi wanashinda Lumumba na Kinondoni.Wakikosa vyeo,hutokea mifadhaiko na kufanya mambo ya kipuuzi.DARUSO na vyama vingine vya wanafunzi ni nusu CCM na nusu CHADEMA.Ndio maana naona ni vema kama inakubalika wakasajili chama cha siasa.

Lakini mchezo huu unaofanywa na vyama vya wnafunzi na washirika wao CCM na Chadema hauna nia jema na Taifa.Taifa haliwezi kuendelea bila kuwa na wasomi waliopikika hasa.Lakini wasomi wetu wanajihusisha na siasa uchwara.

Ni nadra sana kukuta wasomi wetu wa sasa wanafanya migomo kwa sababu za msingi,au hata wanajadili mambo yenye masilahi ya Taifa.DARUSO ni mfano tu wa vyama vya wanafunzi wa elimu ya juu.Ningependa kuwashauri vijana wetu/wanafunzi kujikita zaidi kwenye masomo.Kila kitu kina wakati wake.Jitambeni,jueni wajibu wenu kwa Taifa.Na hawa ndugu zangu akina Nape,waacheni wanafunzi wasome.

IMEANDIKWA NA BABA TUSAJIGWE (MUGO)
MAPAMBAZUKO TANZANIA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…