Kweli hatuna jeshi jama tunashindwa kufanya mambo yetu ndani ya inchi kisa kikosi cha alshababi watu ambao hatujawachokoza kweli hapa naamini tunaishi kwa kudra za mwenyezi mungu mungu tusaidie kutulinda na kila janga kwani hatuna jeshi.
Kama wakizuia maandamano ya wananchi kupinga muswada wa kuandika upya Katiba kutiwa saini kwa kisingizio cha Al-Shabaab basi watanzania tujeukie migomo, tukiaanza na kugomea CECAFA Cup, kwani kama wameshindwa kutulinda katika maandamano watawezaje kutulinda katika burudani? Lazima tutee haki yetu ya kikatiba ya kukusanyika na kutoa maoni yetu!
....Jeshi la polisi limezuhia maandamano yaliyokuwa yamepangwa na JUKWAA LA KATIBA kwa ajili ya kudai haki ya mwananchi maskini aliyefanywa maskini na CCM kushiriki moja kwa moja kwenye hatua za awali za kuunda katiba mpya...Na sababu ni ileile AL-SHABAAB.........Hii ni sababu ya kipumbavu kabisa,jeshi gani lisiloweza kuwalinda wananchi? Mbona kuna mikusanyiko mingi inaendelea hakuna tishio la Al-shabaab? Kama jeshi letu linataka watu wenye akili tuwaelewe naomba tuhairishe MAADHIMISHO YA UHURU WA TANGANYIKA Desemba 9 na SENIOR CHALENJI CUP inayotegemewa kuanza kesho...Ama sivyo tumepoteza imani na hili jeshi.....