DANTE FIT

saimon amos

Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
16
Reaction score
7
Chikupe kuongeza nguvu Yanga dhidi ya Mwadui Fc kesho

Baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili, vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga kesho wanarejea 'mzigoni' kwa kuumana na Mwadui fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania utakaopigwa uwanja wa Taifa kesho Jumanne, Januari 15 2019

Mchezo huo ulirudishwa nyuma kwa siku moja sambamba na mchezo wa ugenini dhidi ya Stand United ambao utapigwa Januari 19 ili kuipa nafasi Yanga kuwahi kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup yanayoanza Januari 22 2019

Katika mchezo huo beki Andrew Vicent Chikupe anatarajiwa kurejea katika kikosi cha Yanga baada ya kupona majeraha.

Chikupe pia ameamaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni VIP A Tsh 15,000/-, VIP B na C Tsh 10,000/- na
Mzunguuko Tsh 5,000/-

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…