Kwa zaidi ya saa nane wakazi wa mkoa wa Morogoro wamekosa huduma ya usafiri wa daladala kutokana na mgomo wa madereva kwa madai ya bajaji kupakia abiria
Kwa zaidi ya saa nane wakazi wa mkoa wa Morogoro wamekosa huduma ya usafiri wa daladala kutokana na mgomo wa madereva kwa madai ya bajaji kupakia abiria kinyume na utaratibu waliowekewa hivyo kuwaathiri kibishara.
Madereva wa daladala wanalalamikia walichodai wingi wa bajaji kunakobabisha wao kukosa abiria na kwamba wameamua kurudisha magari yao kwa wamiliki kutokana na kufanya kazi bila maslahi, ingawa baadhi ya mabasi yameonekana kubeba abiria na kuwashusha katika standi hiyo ya daladala.
Kufuatia mgomo huo wa madereva, mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk,Kebwe Steven Kebwe ameagiza mkuu wa wilaya kutoa elimu kwa kwa madereva wa bajaji ili wafanye kazi kwa mujibu wa leseni zao na wanaokiuka kuchukuliwa hatua stahiki .
Jamaa kakimbia uzi wake asee
Hata sisi bajaji tunalipiaKodi tunalipa sisi tulio kwenye orodha ya walipakodi. Hao Bajaj wanapiga pesa ndefu, lakini hakuna kodi yoyote. Daladalka kodi kibao, teksi kodi kibao, halafu wanaachwa hao wenye bajaj watambe tu. Hakuna usawa hapo. Malalamiko ya daladala ni sahihi.
Kodi tunalipa sisi tulio kwenye orodha ya walipakodi. Hao Bajaj wanapiga pesa ndefu, lakini hakuna kodi yoyote. Daladalka kodi kibao, teksi kodi kibao, halafu wanaachwa hao wenye bajaj watambe tu. Hakuna usawa hapo. Malalamiko ya daladala ni sahihi.
Hata sisi bajaji tunalipia
Sumatra, bima,ushuru wa parking, stika ya manispaa, posho kwa bosi n.k je kwani sisi sio watanzania kama nyie?
Hatuna majukumu kama nyie?
Acheni wivu, uvivu,husuda na roho za chuki kwa wenzio.
Hawa madreva wasenge Sana.. Kwahyo wao peke yao ndio wanataka fursa ila wengne wastahili..
njoeni dar nyinyi
Watu wanaenda kufuatana na mabadiliko ya kimazingira ama teknolojia, sio lazima MTU akae stand masaa kibao kusubiria gari ijae ilihali anahitajika haraka sehemu husika.Great!!
Hoja waliyotoa waliogoma ni ya kitoto kabisa, haina tofauti na wanasiasa wanaosema "watu wangu" mteja ana uhuru wa kuchagua huduma anayotaka, hivi leo hii waarabu wagome kuzalisha mafuta ati kwasababu wameona kuna teknolojia ya magari kutumia umeme!!