Jamani sasa hivi kila mtanzania amebumbuluka na kuwa mjasiri na kujua haki yake. Nipo kijijini msimamo walionao walimu kwa sasa hivi serkali wawe wapole na waangalifu. 1. Ukitangazwa tu mgomo watashiriki kikamilifu zaidi hii ni hasira ya wenzao waliopewa msukosuko mgomo uliopita. 2. Kuhakikisha watoto wao na ndugu zao wa karibu katu hawajikuwa walimu kama wazazi wao. Hii ni long plan. 3. Kumwaga sumu kwa wanafunzi wao ili wakue wakiichukia ccm na serkali yake eti hasa Nape (sijui ni kwa nini.) wako seriously. Propaganda ya kuhusu cwt serkali imechelewa. Wanadai kweli viongozi wengi wa cwt zamani walikuwa mamluki lkn kwa sasa eti wako wachache walio wazalendo. Kwa hiyo watafanya nao hao mapinduzi ili iwe fundisho kwa serkali zote zinazofuata kuwaheshimu walimu..