Timu ya soka ya CRD Libolo ya Angola imeiondoa timu ngumu ya El Mereikh ya Sudan kwenye mashindano ya kombe la klabu bingwa ya Afrika baada ya kuichapa tena mabao 2-1 huko huko Omdurman, Sudan. ikumbukwe kuwa Libolo iliifunga El Mereikh 2-1 walivyokutana Angola, kwa hiyo Libolo wamesonga hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 4-2, na watapambana na mshindi kati ya Kano Pillars ya Nigeria na Vital'o ya Burundi