Eti........bila kapicha, habari hii ni umbea tu!
Si useme ni wewe tu kwani nani anakujua
Wacha nitulie hapa
Uzi tayari
Ni kweli kurekebishana kunajenga, huwa kuna kujifunza ndani yake, hata kama mtu atachukia.R na L nimejifunza kutofautisha humu humu JF.
Waliokua wanakwazika wamenisaidia aisee. Shida wengine standard 1 to 3 ndio tulikua watundu hata shule sometimes hatufiki.
1. Jifunze kuandika kwanza
2.
3.
4. Nimewahi kitu cha mbele
5.
6.
7. Tuwasubiri wake
8.
Mtoa mada umeisahau hii.
Ulichoandika hapo 4 na 7 natamani nikujibu kwa namba 1, sema ndo ushapiga mkwara!
Hata nisipokwambia, hivyo ndivyo ninavyojisikia.
Sawa... !! Lakini usipokubali kukosolewa hutaacha tabia au matendo yasiyofaaHabari wana JF wote kwa ujumla. Kama title inavyojieleza.
Nimeona Leo nianzishe huu Uzi ili wenye hizi tabia waache kwa sababu naamini muda mwengine huwa inawekera baadhi ya waleta mada.
mtu amejipinda kuandika siri zake humu ili apate msaada watu wengine wanaleta mzaha kwa comments zisizo saidia
Au mtu kaandika Uzi mrefu katiririka vitu vya msingi halafu anajikuta anakutana na comments kama zifuatazo :-
1. Jifunze kuandika kwanza
2. Umeandika kama unakimbizwa
3. Sawa
4. Nimewahi kiti cha mbele
5. Au mnasemaje mods
6. Jua kutofautisha kati ya R na L
7. Tuwasubiri wajuvi waje
8. Shule bora zifunguliwe
9. Una miaka mingapi
10. JF kumeingiliwa
11. Nipe namba yake (mtu anaomba ushauri kuhusu mkewe)
Eti........bila kapicha, habari hii ni umbea tu!