CNN: 'Don't use birth control,' Tanzania's President tells women in the country

Wazungu wanajua silaha ya mwisho ya waafrika kuitumia ili kuwatawala ni idadi kubwa ya waafrika..wanahaingaika sana kutupunguza lkn miaka 2000 ijayo wanajua fika kuwa Afrika na waarabu ndo watakuwa wanatawala hii dunia...wacha washtuke
 
Hivi walioambiwa ni lazy ni wanawake au wanaume???.
Wote wanaopanga uzazi ni "lazy" wawe wanaume au wanawake. Kuzaa watoto wengi siyo kigezo cha kushindwa kuwatunza, kuna watu wana mtoto mmoja au wawili na bado wanashindwa kuwatunza. Kupanga uzazi siyo kigezo cha kuwa na familia bora, bali kumheshimu MUNGU na kuitii sauti yake ndiyo mwanzo wa maisha bora!
 
Wazungu wanajua silaha ya mwisho ya waafrika kuitumia ili kuwatawala ni idadi kubwa ya waafrika..wanahaingaika sana kutupunguza lkn miaka 2000 ijayo wanajua fika kuwa Afrika na waarabu ndo watakuwa wanatawala hii dunia...wacha washtuke
Kazana kufyatua baba, haujakatazwa na mtu.
 
Kama kuna tatizo basi ni kusema ukweli. Hakuna jipya hapo, au kwa kuwa ni CNN. Uzazi wa mpango ndo tatizo kubwa la familia zetu kweli? Tukiwadekeza watu hawa, kesho wanalazimisha yale ya Malawi. Kulazimisha kutambua haki za ndoa ya jinsia moja. That is a non issue!
 
Adam na Eva walizaa watoto watatu,kwenye biblia Yakobo tu ndo alikuwa na watoto wengi 12 na aliwapata kutoka kwa wake wawili sasa inamaana watu wa kale hawakuelewa Magu ndo kaelewa sana. Yeye kwanza anao wangapi
Acha kabisa uongo mkuu, tena acha kabisa uongo; Adamu na Hawa walizaa watoto wengi sana isipokuwa tu walioandikwa majina yao walikuwa hao wachache. Soma hapa MWANZO 5:4-5......"Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia tisa na thelathini naye akafa"......hapo kwenye "red" unaona kuwa imeandikwa alizaa "wana waume na wake" hii maana yake kuwa alizaa watoto wengine wengi tu tena wanaume na wanawake. Neno "wana" limetumika kwa wingi.

Hivyo kama Adamu hakuzaa wana wengine mbali ya Abeli, Kaini na Sethi basi isingeandikwa baada ya kumzaa Sethi alizaa wana waume na wake. Mkuu singojr kabla hujakurupuka kuandika kitu kutoka kwenye Biblia hakikisha umesoma vizuri, vinginevyo utakuwa unawapotosha watu.
 
Ndiyo maana na mimi nimesema kuzaliana ni agizo la MUNGU. Hivyo agizo la Rais Magufuli kuwa Watanzania "wazaliane kwa wingi" halina makosa na siyo dhambi watu kuzaliana kwa wingi.
 
MALIZIA HAPO "Tunaweza kweli kweli".
HATA MM SIO TEAM MAGU NA KAMWE SITAKUWA LAKINI HUO NDIO UKWELI KWENYE HILO LA UZAZI NA MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU.
mara nyingine tunakuwa waongo hata kwa vitu vilivyo wazi, utakuta mtu kazaa watoto 2 na mkewe na huko nje amezaa wa3, huko sio kuzaana?
Magu kasema kweli sisi tunazaana kweli kweli lakini tumejaa unafiki hatutaki kuwa wazi
 
Hili la kuzaa ninaunga mkono hoja ya JPM.Russia na baadhi ya nchi za ulaya sasa hivi wapo katika kampeni ya kuongeza idaidi ya watu.Mwenye uwezo na azae kwa hata mungu alisema tuje kuijaza dunia.
kuna vi nchi kama Denmark, Sweden wakiona mtoto kama wameona dhahabu, vizee tu vimejaa, pamoja na kuwa na uchumi mzuri lkn hawewezi kuwa taifa lenye nguvu sababu hawana nguvu kazi, mfano hawawezi kuwa na jeshi kubwa kama China na Usa.
 
Naunga mkono maneno ya Rais 100%.
Kaka Magufuli umepiga msumari kwenye kidonda.
wazungu lzm wachukie. manina zao wacha wafe kwa hasira.
wao wameshazoea kuzaa km Twiga. mtoto mmoja mmoja.
matokeo yake nchi inawashinda kuiendesha mpk wakaombe wahindi na waafrika kuja kusaidia.

hapa ni kuzaana kwenda mbele.
anaekataa akafunge gavana.

wabongo acheni kuwa watumwa wa wazungu. kila wakisemacho mnafuata tu
 
What shame is this. We are looking forward to hearing what policy makers saying. It is not his fault but is ours .
 
Wazungu walikwisha endelea zamani sana tukiwafwata sana tutapotea mfano mzuri ni huu hapa wanatuacha tunapambana na lugha yao huku wao wanasonga mbele ukielewa lugha yao wanakupa na sheria hujamalidha hapo unakufa unawaacha wao cha msingi tufanye yetu tu
 
Kwani Magu alipinga huo mpangilio wa kuzaa? Hapana tusimwelewe vibaya. Yeye alitutaka tuzalishe zaidi ili pia tuweze kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao tutaweza kuwamudu.
 
Si kila jambo ni kuiga western country. Hatuwezi kupangiwa watoto wetu. Sisi tuzae sambamba na kiwango cha uchumi wetu. Mi naona Magu yupo sawa tu.
 
Only fools can be fooled!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…