Unajua nilidhani ni mimi pekee ambaye nachukizwa na tabia ya hawa Clouds kujifanya miungu watu, wanafanya mambo ya kiswahili mpaka wanaboa.
Kampeni yao ya kataa kuwa kaa nilidhani inalenga kuwaunganisha vijana wapeane dili, rakini baada ya Makonda kuwatembelea kuwapa pole, basi wakabadilisha mpasho unaoendana na ugeni huo na kuanza kusema Mashetani tunaishi nayo, yanajifanya mema, niliposikia upuuzi huu, niliamua kunadili stesheni nianze kusikiliza R.F.A japo namkosa Fredwaa aliyekuwa amenifanya nimfate Clouds, muda mwingi niliamini Ruge ni akili kubwa rakini nimeelewa kwanini wanasema ukishindwa kuweka pamoja familia yako, basi usitegemee kuwa mwanaume wa maana.