Labda anahubiri bia huku anakunywa soda. Mi simjui vizuri huyu dada ila siku moja pale moshi nikisubiria show ya ngwasuma akapita na jamaa mmoja watu wakawa wanasema huyu sio diva wa clouds? wakasema ndiye basi mwingine akasema diva ametoka kulipia chumba mapema kati ya zebra au bufalo hotel ili baada ya show wakapumzike. Ninachojua watu wa habari na wasanii ni kioo cha jamii hivyo matendo yake yanweza kuangaliwa pia. Pamoja na hayo yote mimi nadhani ni vyema tusimjadili mtu nguoni, tumjadili utendaji wake maana sidhani kama kuna mtu ambaye nguoni hana udhaifu.