Sasa wangekua wanatangaziana tu ndani kimya kimya kuliko kuleta masihara kwenye mambo ya ajira.Nadhani wanaendesha usaili kama ushahidi tu ili ukaguzi ukipita wapate kujitetea kwamba mchakato wa usaili ulifanyika.Kuna nafasi za Data Officer walifanyisha watu usaili hapa Dar lakini mpaka leo hakuna hata mtu mmoja ninaemfahamu ambae kaitwa kazini.
Kiukweli wana uhuni mwingi sana na inaonekana pale kuna mambo ya kujuana kwa kiwango cha lami.