Clauds FM Vs Super brand

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Posts
3,429
Reaction score
6,393
Nimeshangazwa sana na radio ya Clouds kupewa tuzo ya superbrand wakati regulator analalamikia kituo kirusha content ambazo hazikubaliki kijamii. Je hiyo tuzo wamepewa kihalali?

Ninazohisia kwamba mpaka kufikia kupigwa fine lazima wameshatoa onyo za kutosha kabla ya kuwatoza fine, so hii tuzo imefuata utaratibu wake kweli?

Hivi super brands nini? Vigezo vyake ni vipi? Je kina nani wanatoa maoni ya nani bora zaidi?

Kama jibu ni jamii inayosikiliza radio ama tv au product iliyoingizwa kwenye kinyanganyiro, ni njia gani wanayotumia kupata hayo maoni?

Kama ni kwa njia ya inTerview simu na mitandao ya jamii, kama ndivyo naamini walipita hapa JF.

Hapa JF malalamiko dhidi ya chombo hicho ni mengi saaaaana ikifuatiwa na radio Iman ya morogoro.ambayo nayo imeadhibiwa.


Swali: je CloudsFM wanastahili kweli kupewa tuzo ya super brands? Na Kwa nn sio Radio One, EARadio, Magic, radio free africa, etc?

Tujadiliane kwa uwazi na kwa upana wake.
 
Tungejua vigezo vya super brand tungechangia ila subiri wana jf waje watasema
 



"No research no right to speak" chambilecho wazungu. Kwa kikwetu tolonga "Hakuna utafiti hakuna haki ya kuongea". Kama huna uhakika na mambo ni bora ukakaa kimya kuliko kutoa ushuhuda wa uongo!!! Au ni kwa wee ni miongoni mwa wale wasioipenda clouds fm??!!!!!. Pole sana, unaemchukia ndio kapata tuzo!!
 



Mkuu nakubaliana na wewe

Ila kila sector ilikua na mshindi walau mmoja
upande wa TV = ITV
Upande wa Magazeti = Mwananchi
Upande wa Radio = Clouds
n.k

So bado suali langu linabakia pale pale vigezo ni kuhoji watu 1,800? Je waliwapataje? Je hiyo sample ni representative?
 

Kwani wee ulitegemea radio gani tofauti na clouds fm ndio iibuke mshindi???!! Mbona huoji kwa nini ITV imeibuka mshindi badala ya STAR TV au TBC 1???!! Mie binafsi natumia majani ya chai ya GREEN LABEL TEA!!! Lakini mbona sihoji kwa nini CHAI BORA washinde???!!
 

Mkuu nimehoji kwa sababu moja tu.

ITV haijahi kufungiwa ama kupewa adhabu (fine) hivyo naweza kusema ilistahili
lakini iweje radio inayolalamikiwa na wadau wengi bado inasemwa ni radio bora (superbrand)

inaonekana unakunywa chaibora ya kutoka mara
 
Mkuu nimehoji kwa sababu moja tu.

ITV haijahi kufungiwa ama kupewa adhabu (fine) hivyo naweza kusema ilistahili
lakini iweje radio inayolalamikiwa na wadau wengi bado inasemwa ni radio bora (superbrand)

inaonekana unakunywa chaibora ya kutoka mara

Umetumia kipimo gani kinachoonyesha kuwa clouds fm inalalamikiwa na wadau wengi. Inaonekana wee ni miongoni mwa wale wasiopenda watu fulani nao wapate vitu fulani. Pole sana ndugu.



 
hapa upele umepata mkunaji.!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…