Mimi nadhani kama kuna mtu ana sifa tajwa na anajisikia kuguswa anaweza mtafuta wakazungumza.
Katika utumishi wangu nimejifunza mambo mengi... unaweza wewe ukawa na elimu ila usiwe na uwezo wa kupata hizo kazi au usiwe na kipaji cha ujasiriamali..
Kuna mtu ameiashia kidato cha pili ila ana kampuni yake ya ujenzi ambayo inafanya kazi na halmashauri fulani kwa miradi hadi ya 300+Mil ila ameajiri watu wenye ujuzi ambao wanafanya kazi ipasavyo.
Hivyo hatutakiwi kumbeza mtoa mada.
Nawasilisha