Date::1/14/2009
Daruso yafutwa, sheria mpya UDSM zatangazwa
Latifa Karugila na Hussein Kauli
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeweka masharti magumu ya kudhibiti usajili wa wanafunzi waliodahiliwa upya kuingia chuoni hapo kuanzia Januari 19, mwaka huu.
Vile vile, kimetangaza rasmi kufutwa kwa sheria za chuo zinazotambua kuwepo kwa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (Daruso).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Makamu Mkuu wa chuo (Taaluma), Profesa Makenya Maboko, ilionyesha kuwa wanafunzi wote watakaotimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo, watapewa vitambulisho vipya pamoja na taratibu za namna ya kuishi chuoni hapo.
Profesa Maboko alieleza kwenye taarifa hiyo kuwa, mwanafunzi atakayekutwa ndani ya chuo bila ya kuvaa kitambulisho atakuwa amesababisha uvunjifu wa amani na utulivu, hivyo atachukuliwa hatua za kisheria juu ya kitendo hicho.
"Wanafunzi watakaokuwa wamevaa vitambulisho hivyo ndio watakaoruhusiwa kuingia darasani," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Ili kutekeleza masharti hayo, Profesa Maboko alisisitiza kuwa kila mwanafunzi atakayekamilisha taratibu za usajili atapaswa kupatiwa kitambulisho kipya, vinginevyo hatatambuliwa kama mwanafunzi aliyetimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo.
Akizungumzia kuhusu Serikali ya Wanafunzi wa UDSM (Daruso), Profesa Maboko alisema taasisi zote za wanafunzi zilizokuwa zikitambuliwa na sheria ya chuo ya mwaka 2007, kabla ya kusimamishwa kwao, hazitatambuliwa tena.
Alisema taasisi hizo zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho.
"Taasisi mpya za wanafunzi zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho," aliongeza Profesa Maboko.
Wanafunzi waliosajiliwa upya watatakiwa kuripoti chuoni hapo kuanzia Januari 19 hadi 22, mwaka huu, kwa utaratibu maalumu uliotolewa na chuo.
Source: Mwananchi 15/01/2009
Kosa lingine ni letu wazazi. Vijana wanagoma wakiangalia uwezo wa sisi wazazi wao. Sisi tunakaa kimya kana kwamba hayatuhusu. Tunawasaliti vijana na kwa kufanya hivyo tunajisaliti wenyewe. Tunapaswa kupaza sauti zetu na kumuuliza JK, mbona watoto wa maskini wanakosa elimu wakati ulisema haitatokea hivyo?
Tujiulize pia, hivi watoto wote wanaotaka mkopo wakipewa asilimia 100 kuna shida yoyote? La msingi ni kuwabana walipe, period. Ni kama nataka kulima, naenda benki kukopa, benki inanipa hela za kulimia tu na inasema za kuipanda na kupalilia nijitegemee wakati sina uwezo huo. Je nikilima tu huo mkopo utarudi? Si bora wanikoppeshe hadi gharama za kuvuna na kuuza ili hayo mauzo ndiyo nilipe mkopo?. Serikali tumia akili.
Tatizo linakuwa gumu kwani JK, mkuu wa nchi alitoa msimamo wake mapema sana juu ya suala la sera ya uchangiaji kuwa haitabadilishwa. Ni kosa kubwa kwa rais kutoa misimamo kama hiyo kwani wewe ndiye mkuu kabisa, Sasa tuone kama hatakula matapishi yake.
Akisema sera ibaki hivyohivyo - kala matapishi yake maana watoto wa maskini hawatasoma. akisema ibadilishwe - kala matapishi yake maana alishasema haitabadilishwa. KAZI KWELIKWELI.
mkuu tupo pamoja hapa. Unajua! Wanafunzi wakigoma vyombo vya habari vinakuwa vya kwanza kuwabeza eti hawajui hata sababu wanayogomea, mara wanatumiwa na wanasiasa, tena ohh walafi nk. Hata katuni za akina kipanya utakuta zinawabeza eti wanaomba nyongeza wakati wananchi wengine wako hoi. Tena, hata hapa jf wapo wengi tu. Tuliopita pale mlimani tunajua issue ilivyo na namna 'wazazi' walivyotutosa kutuunga mkono na kuendelea kusikiliza propaganda za serikali.
Sasa unapofuta daruso unataka nini kama siyo kuongeza matatizo? Katika ulimwengu wa leo huwezi kutawala bila kuwashirikisha unaowatawala. Daruso imekuwa ikisolve matatizo mengi ya wanafunzi na kuwawakilisha wanafunzi katika vikao mbalimbali vya chuo kuanzia senete. Hivi utakuja tu kuwaambia wanafunzi kadhaa wamedisco au supp. Bila mwakilishi wao kuhusika seneti?!!! Damn!
Halafu eti mwanafunzi wa chuo kikuu atembee chuoni akiwa amevaa kitambulisho! What a shame!
'wazazi' = wananchi.
kama wanafunzi wa chuo kikuu wanabehave kama watoto wa sekondari basi ni sahihi kuwawekea sheria kama watoto wa sekondari walio kwenye umri wa baleghe. Hawa wanafunzi wamekuwa aibu tupu na migomo yao isiyokuwa na kichwa wala miguu. Hongera uongozi kwa jitihada za kubuni mbinu za kujenga taifa lenye nidhamu, busara na fikra wajibifu.
watu wameanza kuzeeka akili,DARUSO sio chanzo cha vurugu au migomo!
Good, safi sanaDate::1/14/2009
Daruso yafutwa,
Vile vile, kimetangaza rasmi kufutwa kwa sheria za chuo zinazotambua kuwepo kwa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (Daruso).