charger nadhalilika mnisaidie.

charger

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
2,320
Reaction score
1,374
Kama mnavojua januari mambo na mahitaji huwa mengi sana.

Sasa kuna jamaa nilimkopa hela akaahidi atanirudishia mapema lakini sasa Imepita miezi sita hajanirudishia na ananikwepa kila anionapo.Simu zangu hapokei tena.Nimejaribu kumsaka sana kabadilisha njia alizokuwa anapita.

Na habari nilizozipata kutoka kwa watu wangu jamaa amefikia hatua anatembea kwenye van ya kuuzia magazeti ambayo inasimama karibu kabisa na mlango wake,akitoka tu kwenye van anaingia ndani kwake na ikifika sasa 10 alfajiri anatokomea mitaani.

Wenzangu mmeshawahi kukutana na hali kama hii na je mlijikwamuaje?
 
Weka picha yake mkuu utampata leo hii
 
wapo kibao hapa hawana shughuli yoyote ngoja niongee nao wakamuwashe mpaka atie adabu.
Nalog off

Nitafutie wenzio kama 10 hivi wa kiume then tuwasiliane.
 
amka sa kumi na moja kaa mlangoni kwake mpaka usiku asipotoka msamehe tu si ya kwako.....
 
Kama Mbwai-Mbwai bwana, Niuzie kesi mimi-
Atalipa tu.Kamisheni 10% lakini.
Kama uko tayari ni PM kwa Maelezo zaidi.
Fursa ndio hizi watu mnambwelambwela alaaah!
 
Kama Mbwai-Mbwai bwana, Niuzie kesi mimi-
Atalipa tu.Kamisheni 10% lakini.
Kama uko tayari ni PM kwa Maelezo zaidi.
Fursa ndio hizi watu mnambwelambwela alaaah!
Mkuu utamuweza huyo jamaa?
 
Kama Mbwai-Mbwai bwana, Niuzie kesi mimi-
Atalipa tu.Kamisheni 10% lakini.
Kama uko tayari ni PM kwa Maelezo zaidi.
Fursa ndio hizi watu mnambwelambwela alaaah!

umeniwahi, ila nawe ikikushinda niuzie kesi, nnauzoefu wa hayo mambo.
Au kama vipi tushirikiane then tukishaipata nasi tunamtapeli.
Charger yenyewe ya pin ndogo, haiwezifanya kitu.
 
Huyo jamaa kama yumo jf tena akipata kusoma huu uzi, ataamka saa nane
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…