Habarini wakuu.
Sijui kama namna nilivyo weka kichwa cha uzi wangu kitakua sahii sana, japo lengo la uzi huu linabeba maana sawa na hiyo heading. Niende sasa kwenye content niliyokusudia.
Imekua tamaduni kwa vijana wengi katika malezi yetu tumekua tukiamini kwamba kupitia kusoma na baadae kuajiriwa tutaweza kujikwamua kimaisha na kusaidia familia zetu ambazo zinatutegemea.
Hali imekua tofauti kidogo kwa miaka ya hivi karibuni ambapo tumeshuhudia wimbi kubwa sana la vijana waki hitimu elimu na wanakosa nafasi za ajira, nadhani ni kutokana na ufinyu wa fursa za ajira zinazotengenezwa. Hata hivyo kwa nafasi chache ambayo zimekua zikitokea bado kumekua na nguvu kubwa ya nani anakujua ili upate nafasi (CONNECTION).
Mbaya zaidi hata njia mbadala ya kujiajiri bado imekua changamoto kwa wengi kutokana na kukosa uzoefu na misingi mizuri ya biashara na hata ule ujuzi mbadala kwa vijana wengi ni tatizo.
Binafsi ni kijana nilie hitimu Degree ya land management na valuation. Bahati mbaya sikua najua chochote kuhusu hii kozi wakati naichagua ila kilicho nisukuma kuichagua ilikua ni kupata mkopo ili niweze kusoma na pia kuamini kwamba kozi ambayo zinapewa kipaumbele kwenye mkopo ajira zake zinapatikana kiurahisi lakini baada ya kuhitimu mambo yamekua tofauti na mbaya zaidi ni kwamba sikua na connection ya kuwafahamu watu wa kwenye hii industry sasa hata kupata fursa kwenye private company imekua changamoto.
Waswahili wanasema kuanza upya si ujinga na uwezi jua wapi utakutana na mtu anae weza kukusaidia, naomba kutumia uzi huu japo kuomba fursa kwa watu mbalimbali ambao kwa namna moja wanaweza kua msaada.
Kwanza kabisa watu wa bank (MAAFISA MIKOPO), kupitia watu hawa naweza kufanya nao kazi katika kipengele cha valuation za mortgage. Maana hata kuwapata wao imekua inahitaji connection.
Pili ni makampuni binafsi ambayo yana assets zake na uwa wanahitaji mtu wa kuwafanyia tathimini ya thamani kwaajili ya financial issues na hata kuuza au kununua, mfano makampuni ya ujenzi na viwanda. Na mwisho kama nitapata connection ya valuation firm ambayo inaupungufu wa vijana.
Mbali na kazi za professional pia kama napata connection ya kazi nyingine pia nipo tayari kufanya kwasababu mwisho wa siku matarajio yetu ni kufanikiwa kimaisha haijarishi tutafanikiwa kupitia vile tulivyovisomea.
Pia naomba nitumie uzi huu kuwaomba ambao angalau wana nafasi wajitahidi japo kuwagusa vijana walioko mtaani kama mimi ambao wana struggle kuona namna gani wanajikwamua ili wanakutana na changamoto kadhaa ikiwemo hii ya kukosa connection.