Nachagua kuwa decision maker katika wizara ya elimu. Nitapenda kuona mfumo na mitaala ya elimu hasa primary na secondary inabadilika kumfanya wahitimu wawe chachu ya mabadiliko endelevu na maendeleo katika jamii zao.
Hivi sasa tunawaona vijana ambao hawajaweza kuchaguliwa kuendelea darasa la 7 au form 4 kama wameshindwa/failures. Mtazamo huu ni wa kinyanyapaa na naona badala ya kuwaita vijana hawa failures serikali ndio inawajibika kwa kushindwa kwao. Kwa Vission yangu itakuwa kutoa elimu ambayo itawasaidi hata wale ambao hawajafanya vizuri
Mtaala wa elimu nitakaopendekeza ni kumuwezesha mwanafunzi anayemaliza kuwa basic elimu kwa nadharia na vitendo ya kumudu mazingira yake.
Binafsi sioni sahihi kwa mwanafunzi wa shule ya monduli kumaliza darasa la saba au form4 bila kuwa na somo la ufugaji japo kwa mwaka 1ja.Sioni sababu kwa sahihi kwa mwanafunzi wa wilaya ya ukerewe asifundishwe somo la uvuvi. Sioni sababu kwa nn mwanafunzi wa lushoto amalize shule bila na elimu ya nadharia na vitendo ya kilimo cha matunda na mboga mboga.
Nina hakika kila wilaya inaweza kuwa na somo moja ambalo linaendana na mazingira ya sehemu husika. Wanafunzi watafundishwa somo hili darasa la sita na la saba vile vile kwa form 3 na form 4.
Njia za kupata walimu wa masomo husika kwa kuanzia zinaweza kutumika njia kama za upe . watu wa maeneeo husika wenye ujuzi asili wa taaluma husika watapigwa msasa na watatumiwa kuwafundisha wanfunzi. Itakuwa ni jukumu la serikali kuandaa mitaala ya masomo haya.
Nahakika kwa mabadiliko haya jamii na serikali kwa ujumla itapata faida zadi ya sasa ambapo tumekazania kwenye elimu ya kawafanya wnafunzi wafanye white collar jobs.