Viwanja vyenye ft 50 kwa 50 vinauzwa chamazi, kila kiwanja kina angalia barabara, maji na umeme upo. Bei ni 7m. Ni vyangu mwenyewe sio dalali mawasiliano kwa atakayetaka 0681004080
Mkuu,
Jaribu kua wa kisasa zaidi. Futi 50 ni sawa na Mita 15 tu, unafikiri kinatosha??.
Watu wanataka viwanja waweze kuweka labda Nyumba kubwa na banda la kuku kwa uwani, bustani kwa mbele, kiuwanja kidogo cha kuchezea watoto n.k., vitatoka wapi hivi kwenye Mita 15 square??
meter 15.24 kwa meter 15.24 mil 7?
15.24m x 15.24m = 232m[SUP]2[/SUP]
232m[SUP]2[/SUP] = Tshs 7,000,000/=
1m[SUP]2[/SUP] = Tshs 30,200/=
Tena chamazi..!
Ukipiga kwa heka nzima ambayo ni approx 4000 sqM utapata almost 120,000,000. Duh, ardhini kuna mgodi/ madini nini.?
....meter 15.24 kwa meter 15.24 ......... Bei ni 7m.
Sema kuwa wewe huwezi, mbona vinanunuliwa? Kuhusu umbali muulize google. Siku za jpili hakunafoleni kabisa natumia dk 25 kutoka chamazi mpaka stesheni. Sihangaiki na maji ya mgao, nimechimba na ni maji safi, ujenzi wake si mgumu huitaji kupasua miamba kukolevel hakuna milima wala mabonde, barabara mpya inayobuniwa ya kutoka airport to kigamboni kupitia chamazi na kongowe inapita ktk eneo hili, kuna faida nyingi sana kwa watu wanaona mbali. Mwenye macho na aone, na mwenye ufahamu afahamu.Afadhali wewe useme mkuu maana!! Hiyo bei sio,utafikiri kiwanja kipo oysterbay
Mkuu hutopata wateja,labda nikupe sababu kama hutojali,kwanini ninunue kwako ambapo hujapima kwa bei ya Tsh 30000 wakati kigamboni Kiwanja kimepimwa bei ni 8500 mpaka 10000,ikizid Sana 15000 au 20000.Nafikiri inabidi ufikirie upya,na huko chamazi ni mbali sana ikilinganisha na kimbiji kigamboni hiyo km 16 sijui umepima tokea wapi
Vitapungua tu bei, 2015 vitapatikana kwa 3m tu
15.24m x 15.24m = 232m[SUP]2[/SUP]
232m[SUP]2[/SUP] = Tshs 7,000,000/=
1m[SUP]2[/SUP] = Tshs 30,200/=
kila la kheri...nasikia wengi wanakimbilia kibaha square mita 1 sh 5000. Mita 30 kwa 30=square mita 900 ambayo ni sawa na sh mil 4.5
na vimepimwa