Chama vis-a-vis Serikali

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Imekuwa kawaida kwa viongozi wa CCM 'kuwaagiza' viongozi wa Serikali mahali wanapotembelea. Utamsikia Nape Nnauye,Abdurahman Kinana Mwigulu Nchemba na wengineo wakisema : ' Naiagiza Serikali....................au namwagiza Waziri/Mkuu wa Mkoa/Mkuu wa Wilaya/Mkurugenzi wa Mji nk.....................'

Je,ni kweli kuwa viongozi wa chama kitaifa wana mamlaka kuliko viongozi wa kiserikali kitaifa?

Mwenye kujua anakaribishwa kunijuza na mimi
 
Last edited by a moderator:
Unatumia akili kidogo tu. Kiongozi yeyote aliyeko madarakani kwa serikali ya Tanzania dhamana zao zipo kwenye chama chao CCM ndiyo hao akina Nape. Sio utaratibu wanavyofanya lakini wanatumia sababu hapo juu.
 
Kusema kweli hilo jambo hatamimi linanishangaza sana. Nafikiri kwa dunia ya sasa ni tanzania tu yenye mfumo huo, kwani kwa kawaida chama cha siasa jukumu lake linaishia kwenye kushinda uongozi wa kisiasa na kuunda serikali na baada ya hapo majukumu ya kutawala ni ya serikali iliyoundwa. Sasa hili la chama cha siasa kufanya kazi za utawala sijui ni kutoka kwenye katiba gani.
 
Bila shaka hali hii imetokana na tanzania kutawaliwa na chama kimoja cha siasa kwa muda mrefu, ukizingatia nchi hii ilikuwa inafuata misingi ya kukifanya chama kushika hatamau, sasa hawa ndugu wamebweteka na yale mazoea, wanasahau kuwa huu sasa ni mfumo tofauti wa vyama vingi vya siasa. Ndio maana watangazaji kama salum mkambala wa magic fm anaposoma gazeti la uhuru asubuhi utasikia "hivi sasa nimelikamata gazeti la chama" hapo anaamini kabisa kuwa kwa yeye anaposema chama basi ni ccm. Kwa kweli wanatakiwa waende na wakati uliopo.
 
Kimsingi wako sahihi tatizo liko kwenye nyakati jambo linalowafanya wasiwe sahihi kwa sasa but nani amfunge paka kengelele kaka mwenyekiti ambae ndio president anaongoza kikao kinachotoa maagizo kwa serikali ambapo president ndio mkuu wake watakosaje watajwa mamalaka hayon ya kuagiza serikali?.
 
Wana JF majibu ya hiyo mikanganyiko yote ni katiba mpya na siyo vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…