PostGE2025 Chama cha Mawakili wa serikali chalaani vikali vurugu na maandamo ya Oktoba 29, wadai maandamano hayakuwa halali

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kinalaani vikali vurugu, mauaji, na uharibifu wa mali vilivyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, na kinatoa pole kwa wote waliopoteza ndugu au mali. TPBA inaunga mkono agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kufanya uchunguzi wa kina na kuwawajibisha wahusika wote kwa mujibu wa sheria.

Katiba ya 1977 inatambua haki za binadamu kama uhuru wa maoni na maandamano, lakini haki hizo zina mipaka ya kisheria kulinda amani na usalama wa taifa. Maandamano ya tarehe 29 Oktoba 2025 hayakuwa halali, kwani yalikiuka zuio la Polisi na kusababisha vurugu.

TPBA inasisitiza kuwa matumizi ya nguvu na silaha yanapaswa kuwa ya kiwango cha lazima pekee na kwa uwajibikaji wa kisheria. Kuhusu changamoto za intaneti, mamlaka zinaweza kudhibiti mawasiliano kwa muda kwa mujibu wa sheria kulinda usalama wa taifa.

Chama kinakumbusha kuwa haki huambatana na wajibu wa kuheshimu Katiba na mamlaka halali. Vyama vya siasa vilivyohusishwa na vurugu vinaweza kufutiwa usajili kwa mujibu wa sheria.

TPBA inatoa wito wa utulivu, umoja, na mazungumzo ya maridhiano kama alivyoeleza Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya Rais, ili taifa liendelee kuwa mfano wa amani barani Afrika.

Imetolewa na:
CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI TANZANIA (TPBA)
 
Alah Haula------------
VIFO Zaidi ya 10,000 halafu Taifa Liwe Mfano wa Amani Afrika------- hawa ndiyo Wasomi wa Serikali ya URT = United Republic Of Tanzania! Tanzania haiwezi kurudi iwe kama ile ya Nyerere... Samia na Vasco Dagama wametufikisha hapa
 
Gen Z fuatilieni hicho chama ofisi zake zipo wapi ili hiyo D9 waende kusalimiwa.
 
Wangekaa kimya tu! Hata pole kwa wafiwa hamna!!?
 
Hutegemei kusikia chochote tofauti na hicho kutoka kwenye hilo kundi la mashetani.
Hicho chama cha mawakili wa serikali kinajumuisha mashetani yanayounda kundi la kuwabambikia kesi watu wanaodai haki, unategemea nini kutoka kwao?

Nchi ikija kujikomboa, hayo ndiyo ya kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kupindisha haki kwa dhamira mbaya.
 
Wapumbavu kabisa hawa.
 
Faki ze mazafakas!
 

Mawakili Ubwabwa hawa. Wao tatizo ni maandano tu. Waliouawa kwao ni by the way. Ni matokeo tu ya maandamano haramu.
 
TPBA inasisitiza kuwa matumizi ya nguvu na silaha yanapaswa kuwa ya kiwango cha lazima pekee na kwa uwajibikaji wa kisheria.
Ngoja kwanza sijaelewa au nimesoma vibaya... ngoja nibaki na LHRC na TLS at least kuna jambo wamefanya la maana nyinyi TPBA sijawaelewa... sawa yaan ndio uue na nyinyi kabisa mna-support mauaji? Nani anawajibika sasa hapo baada ya kuua mtajeni anaewajika kwa kuua wale watu
 
Chama kinakumbusha kuwa haki huambatana na wajibu wa kuheshimu Katiba na mamlaka halali.
Wajibu wa kuua? Katiba ndio inasema watu wakiandamana uwaue? Kuna haki gani na walioua wapo na wanajulikana na hawajafikishwa popote? Au nyinyi pia ndio mlio-engineer yale mauaji?
 
Sycophantic statement by crazy sycophants
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…