Asante kwa mawazo yako. Ugali nimejaribu hapendi. Kuna siku nilipika ndizi za nazi akajaribu kidogo kesho yake nikampikia zake kidogo hakula. Wali wetu hawezi kutafuna bado so nampikia mchele wake laini kuna saa naufanya uji anakunywa na kuna saa naufanya mzito anakula na mchuzi. Wali anapenda. Ila ndo katika hivyo vichache anavyokula. Matunda anapenda mengi tu kama parachichi, embe, ndizi mbivu, papai kidogo, water melon na nanasi. Parachichi amekuwa anakula sana kwa kuwa naweza kulichanganya na chakula kama viazi ili ale some starch maana zaidi ya huo mchele na uji wa dona wenye karanga hakuna starch nyingine anayokubali kwa sasa. I tried oats, boga hadi mkate hapendi piaSwali,je mkimpa chakula mnachokula nyinyi wakubwa anakula au pia hapendi? Wangu alikataa vyakula vya kusagiwa lakin ukimpa hivi vyetu especialy ugali anakula vizuri tu,
Muhimu musimpe vyakula mnavyopenda nyinyi mpeni chochote ambacho anapenda na kula vizuri,matunda mjaribu ya aina yote uone yepi anapenda yepi hapendi
Asante sana. Nipo arusha kidogo nitapita hapo aisee asante sana64Bits Umesema anapenda uji wa mahindi na mchele, mpe huo huo tumia brown rice na mahindi usikoboe ukiweza tumia mahindi ya njano.
Kuna unga wa mchicha nafaka una virutubisho vyote vinavyohitajika na mwili wa binadamu hasa watoto kwa ukuaji bora. Unaweza ukatengeneza uji wake au ukachanganya na hivyo vyakula anavyovipenda. Unaweza ukaweka kama tui la nazi kwenye mchuzi wake ale na wali. Matumizi ni mengi ukigoogle GRAIN AMARANTH utajifunza zaidi.
Nimeshuhudia mabadiliko makubwa kwa watoto kama wanne baada ya wazazi wao kuanza kuwapa huo mchicha nafaka. Appettite iliongezeka na hata wakabadili tabia za kula. Hata watoto wangu ninawapa wataalamu wanasema ni mlo kamili.
Kama uko Arusha unapatikana makumbusho ya azimio la Arusha, unaweza wapigia simu 0786 970 700 au 0759 492 668. Do your research lakini