Mkuu, kwa kawaida, wakati ndege inalelekea kwenye njia ya kurukia; sekunde chache kabla haijapaa; abiria hufahamishwa mambo kadhaa kama vile rubani atakirusha chombo futi ngapi juu ya usawa wa bahari, jotoridi nje ya ndege linategemewa kuwa kiasi gani pindi ikifikia kasi ya juu zaidi na kasi yenyewe itakuwa ipi.
Pia, inategemea kuwasili muda gani huko iendako, inategemewa kupitia katika mawingu manene kiasi gani, pepo na dhoruba kiasi gani na masuala mengine yote ya kiusalama kama milango ya dharura ilipo na namna ya kuifungua, life jackets na nanma ya kulivyaa, n.k.
Sasa basi, kwa kuwa umesema Chadema inazidi kupaa, kwa muktadha huo hebu tupe tips za huko tuendako na issue za kiusalama endapo chombo kitakorofisha njiani.